MITAFARUKU, chuki, masimango, ugomvi na fitina ni vitu ambavyo vimetawala katika sekta mbalimbali za uongozi wa michezo nchini, hususan soka.
Limekuwa jambo la kawaida kusikia viongozi wawili wa juu wa Kamati ya Utendaji ama ya klabu, au chama cha soka kutoelewana kiasi cha kufikia kufanyiana chuki, masimango, majungu na fitina.
Hao ni watu ambao kwa pamoja wamepewa dhamana ya kuongoza chombo na wanachama kwa matarajio makubwa kabisa ya kuleta maendeleo.
Kwa sababu hiyo, huwezi kustaajabu miaka inakatika lakini soka ya Tanzania haipigi hatua kwenda popote.
Rais Jakaya Kikwete amekuwa akitumia msemo wa “Tunajenga nyumba moja, kwa nini tugombee fito” mara kadhaa katika kuwasihi viongozi wa vyama vya upinzani kutovuka mipaka katika upinzani wao.
Ndiyo, maana yake kuna wakati wakubwa wa vyama vya upinzani wanajisahau kwamba wao ni wapinzani wa CCM, na kujikuta wanafanya mambo ambayo yanawafanya waonekane ni wapinzani wa taifa.
Vivyo hivyo, katika sekta ya michezo nchini, hali imekuwa mbaya- upinzani umevuka mipaka na watu wanasahau kwamba wao ni wapinzani wa viongozi waliopo madarakani, wanajikuta wanafanya mambo yanayowafanya waonekane wapinzani wa vyama au klabu zao wenyewe.
Mfano mdogo tu, pale Simba SC inadaiwa kuwa kundi linaitwa Ukawa, ambalo chimbuko lake ni Taliban, hao ni wapinzani wa uongozi wa klabu, chini ya Rais Evans Aveva.
Lakini tuhuma wanazopewa na uongozi, sasa zinafanya waonekane si wapinzani wa Aveva tu, bali wapinzani wa Simba SC pia.
Hiyo ni sehemu ndogo sana ya mjadala katika makala yangu ya leo- kubwa ambalo ni mada mahsusi ya leo.
Tuna matatizo makubwa katika sekta ya michezo nchini na hayo ndiyo yanayoturudisha nyuma kwa kiasi kikubwa- na tusitarajie kwa mtindo huo zile tunazoziita enzi zitarudi.
Katika kila mchezo nchini watu wanakumbuka zamani tu. Katika ngumi, watu wanakumbuka enzi za akina Titus Simba (marehemu), Habib Kinyogoli na angalau wakati wa akina Matumla.
Katika Riadha pia, watu wanakumbuka enzi za akina Juma Ikangaa, Zebedayo Bayo, Filbert Bayi na angalau wakati wa akina Francis Naali.
Na ukija kwenye soka, watu wanakumbuka zamani tu. Zikianza stori za wachezaji wa zamani watu wanakesha. Hakuna jema la kuzungumzia hivi sasa?
Na hali hii itaendelea hadi lini. Lazima tubadilike. Lazima watu wafanye kazi kwa umoja, ushirikiano, amani na upendo.
Lazima ifike wakati watu waaminiane katika kazi. Lakini sivyo ilivyo sasa, watu wanapigana majungu usiku na mchana. Na muda huo huo wanaoutumia kupigana majungu, ndiyo huo huo wangeutumia kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo nchini.
Watu wanapewa dhamana, wakishindwa na kuondolewa, eti wanaingia msituni kuhakikisha wapya walioingia madarakani hawafanikiwi. Na kweli, watawafanyia hujuma ili tu wafeli. Huyo huyo, kesho anajinasibu; “Mimi Yanga damu”, ama “Mimi Simba damu” au “Mimi Azam wa kufa ”. Unafiki mtupu. Na ndiyo maana kila siku watu wanakumbuka zamani tu.

.png)
0 comments:
Post a Comment