• HABARI MPYA

    Thursday, March 05, 2015

    MAN CITY BADO ‘WAMO WAMO’ MBIO ZA UBINGWA ENGLAND, WAIBUTUA 2-0 LEICESTER

    MABINGWA watetezi, Manchester City wameonyesha bado wamo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leicester City Uwanja wa Etihad usiku huu.
    Katika mchezo huo, ambao kocha Manuel Pellegrini alimuweka benchi Nahodha Vincent Kompany, David Silva alianza kuifungia Manchester City kipindi cha kwanza kabla ya James Milner aliyetokea benchi kufunga la pili zikiwa zimesalia dakika mbili.
    Chelsea inaendelea kuongoza Ligi Kuu England kwa pointi zake 63 za mechi 27, Manchester City ya pili kwa pointi zake 58 za mechi 28 na Arsenal ya tatu kwa pointi zake 54 za mechi 28, wakati Man United ni ya nne kwa pointi zake 53 za mechi 28 pia.
    Kikosi cha Man City kilikuwa; Hart, Sagna, Mangala, Demichelis, Kolarov, Navas, Toure, Fernando, Silva/Lampard dk79, Aguero/Dzeko dk85 na Bony/Milner dk72.

    Leicester City; Schwarzer, Simpson, Huth, Morgan, Upson, Konchesky/Nugent dk57, Mahrez/Ulloa dk77, James, Cambiasso, Schlupp na Kramaric/Vardy dk58.
    Spanish midfielder Silva jumps and punches the air to celebrate giving City the lead while Schwarzer (left) lets out his frustrations
    David Silva akiruka kushangilia baada ya kuifungia Man City dhidi ya Leicester City Uwanja wa Etihad

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/article-2979738/Manchester-City-2-0-Leicester-David-Silva-James-Milner-strike-maintain-title-push-captain-Vincent-Kompany-benched.html#ixzz3TTFx3qSV 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY BADO ‘WAMO WAMO’ MBIO ZA UBINGWA ENGLAND, WAIBUTUA 2-0 LEICESTER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top