• HABARI MPYA

    Thursday, March 05, 2015

    LIVERPOOL SASA ‘WAIPUMULIA MGONGONI’ MAN UNITED, NI BAADA YA KUILAZA 2-0 BURNLEY

    TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya vibonde, Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield usiku huu.
    Jordan Henderson alifunga bao la kwanza kipindi cha kwanza kabla ya Daniel Sturridge kufunga la pili kipindi cha pili.
    Matokeo hayo, yanaifanya Liverpool sasa isogee  nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kufikisha pointi 51 za mechi 28 nyuma ya Manchester United yenye pointi 53 za mechi 28.
    Chelsea inaendelea kuongoza Ligi Kuu England kwa pointi zake 63 za mechi 27, Manchester City ya pili kwa pointi zake 58 za mechi 28 na Arsenal ya tatu kwa pointi zake 54 za mechi 28.
    Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can, Skrtel, Lovren, Lallana, Henderson, Allen, Moreno/Toure dk73, Sterling, Sturridge/Johnson dk82 na Coutinho.

    Burnley; Heaton, Trippier, Shackell, Keane, Mee, Arlfield, Jones, Boyd, Kightly/Wallace dk52, Barnes/Vokes dk66 na Ings/Jutkiewicz dk90.
    Liverpool midfielder and vice-captain Jordan Henderson (left) celebrates scoring the opening goal for his side against Burnley 
    Liverpool midfielder and vice-captain Jordan Henderson (left) celebrates scoring the opening goal for his side against Burnley 

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2979963/Liverpool-2-0-Burnley-Jordan-Henderson-Daniel-Sturridge-wrap-confident-win-Reds-Brendan-Rodgers-men-step-chase-Champions-League-football.html#ixzz3TTCg7FId 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL SASA ‘WAIPUMULIA MGONGONI’ MAN UNITED, NI BAADA YA KUILAZA 2-0 BURNLEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top