• HABARI MPYA

    Thursday, March 05, 2015

    ARSENAL WANAMEREMETA ENGLAND, QPR AFA 2-1 NYUMBANI KWAKE

    ARSENAL imeng’ara katika Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Queens Park Rangers Uwanja wa Loftus Road usiku huu.
    Olivier Giroud aliifungia The Gunnes bao la kwanza dakika ya 64, kabla ya Alexis Sanchez kuongeza la pili dakika ya 69. 
    Queens Park Rangers ilipata bao la kufutia machozi dakika ya 82 kupitia kwa Charlie Austin na Arsenal sasa inatimiza pointi 54 baada ya kucheza mechi 28.
    Chelsea inaendelea kuongoza Ligi Kuu England kwa pointi zake 63 za mechi 27, Manchester City ya pili kwa pointi zake 58 za mechi 28 na Manchester United ni ya nne kwa pointi zake 53 za mechi 28.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Ospina, Bellerin, Mertesacker, Gabriel/Koscielny dk36, Gibbs, Cazorla, Coquelin, Rosicky, Ozil/Welbeck dk94, Sanchez na Giroud.

    QPR; Green, Furlong, Onuoha/Hill dk45, Caulker, Yun, Phillips, Henry, Sandro/Kranjcar dk57, Hoilett, Zamora na Austin.
    Giroud lifts Arsenal team-mate Tomas Rosicky up in the air in celebration of his goal shortly after the hour mark 
    Olivier Giroud akiwa amemuinua mchezaji mwenzake wa Arsenal, Tomas Rosicky kushangilia baada ya kufunga bao

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2979784/QPR-1-2-Arsenal-Olivier-Giroud-Alexis-Sanchez-strike-R-s.html#ixzz3TT90mrhP 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL WANAMEREMETA ENGLAND, QPR AFA 2-1 NYUMBANI KWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top