• HABARI MPYA

    Sunday, March 08, 2015

    ILIANZA YANGA B KUSHUGHULIKIWA, IMEPIGWA NNE NA SIMBA B

    TIMU ya vijana ya Simba SC imewafunga wapinzani wao, Yanga SC mabao 4-2 katika mchezo uliofanyika mchana wa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mchezo huo wa utangulizi kabla ya timu za wakubwa za klabu hizo kumenyana katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ulishuhudiwa na maelfu ya wapenzi wa timu hizo waliowahi uwanjani.
    Mabao ya Simba SC inayofundishwa na kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Nico Kiondo yalifungwa na Ibrahim Suleiman dakika ya tatu, Issa Abdallah dakika ya 41 na 51 na Mbarak Yussuf dakika ya 72.
    Kiungo wa Simba B, Mohammed Kijiko akipasua katikati ya wachezaji wa Yanga B leo Uwanja wa Taifa
    Mohammed Kijiko akimtoka beki wa Yanga B, Issa Ngao 
    James Msuva wa Simba B akimtoka beki wa Yanga B
    Makocha wa Yanga B, Salvatory Edward kulia na Nsajigwa kushoto katia benchi lao leo

    Mabao ya Yanga SC inayofundishwa na kiungo wake wa zamani, Salvatory Edward anayesaidiwa na beki wa zamani wa timu hiyo, Nsajigwa Shadrack yamefungwa na Amos dakika ya 57 na Sospeter dakika ya 72. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ILIANZA YANGA B KUSHUGHULIKIWA, IMEPIGWA NNE NA SIMBA B Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top