CHELSEA imezidi ‘kula bata’ siti ya mbele kwenye dege la Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya West Ham United Uwanja wa Upton Park usiku huu.
Shukrani kwake kiungo Mbelgiji, Eden Hazard aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 22 akimalizia krosi ya Ramires kumtungua kipa Adrian.
Kikosi cha Jose Mourinho pamoja na kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa katika mechi saba, pia kinaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi, dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City zikiwa zimebaki mechi 11 kumaliza ligi.
Chelsea imefikisha pointi 63 baada ya mechi ya 27, wakati Manchester City inashika nafasi ya pili kwa pointi zake 58 za mechi 28, Arsenal ni ya tatu kwa pointi zake 54 za mechi 28 pia na Manchester United ni ya nne kwa pointi zake 53 za mechi 28.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Zouma, Fabregas, Ramires, Oscar/Willian dk74, Hazard/Remy dk96, Costa/Drogba dk90+3.
West Ham; Adrian, Jenkinson, Tomkins, Reid/Collins dk7, Cresswell, Noble, Nolan, Downing, Kouyate/Nene dk87, Valencia na Sakho.
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2979941/West-Ham-0-1-Chelsea-Eden-Hazard-heading-big-prize-Blues-maintain-title-advantage-London-derby-win.html#ixzz3TT3PR45w

Eden Hazard akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao pekee dhidi ya West Ham
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2979941/West-Ham-0-1-Chelsea-Eden-Hazard-heading-big-prize-Blues-maintain-title-advantage-London-derby-win.html#ixzz3TT3PR45w

.png)
0 comments:
Post a Comment