• HABARI MPYA

    Thursday, March 05, 2015

    ASHLEY YOUNG APIGA BAO BADO DAKIKA MOJA MAN UNITED YAILAZA 1-0 NEWCASTLE ST JAMES

    BAO pekee la winga Ashley Young dakika ya 89, limeipa ushindi wa ‘zali la shetani’ Manchester United baada ha kuilaza 1-0 Newcastle United Uwanja wa St James Park usiku huu.
    Pamoja na ushindi huo, Mashetani Wekundu wanabaki nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa pointi zao 53 walizovuna katika mechi 28.
    Arsenal ni ya tatu kwa pointi zake 54 za mechi 28 pia, wakati Manchester City ni ya pili ikiwa na pointi 58 za mechi 28, huku Chelsea wakiwa ‘wamejinafasi’ kileleni kwa pointi zao 63 za mechi 27.
    Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Valencia, Evans, Smalling, Rojo/Carrick dk89, Blind, Di Maria/Januzaj dk59, Fellaini/Mata dk82, Herrera, Young na Rooney.

    Newcastle; Krul, Janmaat, Williamson, Coloccini, Taylor/Gutierrez dk64, Obertan, Abeid, Sissoko, Ameobi/Gouffran, Riviere/Perez dk59 na Cisse.
    Ashley Young akishangilia baada ya kuifungia Man United bao la dakika za lala salama ikishinda 1-0 ugenini dhidi ya Newcastle United

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2979709/Newcastle-United-0-1-Manchester-United-Ashley-Young-scores-winner.html#ixzz3TSxW3lIC 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ASHLEY YOUNG APIGA BAO BADO DAKIKA MOJA MAN UNITED YAILAZA 1-0 NEWCASTLE ST JAMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top