MSHAMBULIAJI wa Swansea, Bafetimbi Gomis alizimia ghafla Uwanja wa White Hart Lane na kukumbushia tukio la Fabrice Muamba Machi mwaka 2012.
Akiwa hayupo karibu na mtu yeyite, nyota huyo wa Swansea alionekana kupoteza nguvu katikati ya Uwanja wa kuanguka muda mfupi baada ya Nacer Chadli kuifungiua bao la kwanza Tottenham katika ushindi wa 3-2.
Madaktari wa pande zote mbili waliingia uwanjani kumtibu mchezaji huyio mkali huyo wa nabao.
Bafetimbi Gomis akiwa amezirai uwanjani wakati Swansea ikimenyana na Tottenham
Gomis akitolewa nje ya Uwanja wa White Hart Lane
Gomis alitibiwa kwa dakika tano kabla ya kupelekwa nje akiwa amewekwa kifaa cha kupumulia mdomoni mwake na kupelekwa moja kwa moja katika zahanati ndogo ya Uwanja wa White Hart Lane kwa matibabu zaidi.
Pamoja na hayo, habari njema kwa mashabiki Swansea ni kwamba Gomis alipata nafuu baada ya tiba n a hakulazwa.
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2979806/Bafetimbi-Gomis-collapses-pitch-Swansea-game-against-Tottenham.html#ixzz3TTO2ytzs


.png)
0 comments:
Post a Comment