• HABARI MPYA

    Wednesday, March 04, 2015

    INZAGHI ACHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA AC MILAN

    KOCHA wa klabu ya AC Milan Filippo Inzaghi akatimuliwa endapo atashindwa kuiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi katika mechi dhidi ya Hellas Verona itakayopigwa kwenye uwanja wa San Siro jumamosi hii.
    Baada ya hapo awali tetesi za kufukuzwa kocha huyo kuenea hatimaye taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimetoa uthibitisho kwa kusema kuwa wanampango wa kutafuta kocha mwingine ili aje kuchukua mikoba ya Inzaghi ambaye amekuwa akisusua tangu msimu huu uanze.

    AC Milan inashika nafasi ya 10 katika ligi ya Serie A na hivyo kumfanya raisi wa klabu hiyo Silvio Berlusconi kupoteza uaminifu  kwa kocha huyo ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo.
    Pia uongozi mzima wa klabu hiyo umeonekana kutoridhishwa na mbinu ambazo anatumia kocha huyo na muendelezo wa matokeo mabaya katika klabu hiyo msimu huu.
    Filippo Inzaghi alichukua mikoba hiyo June 2014 kutoka kwa mchezaji mwenzake wa zamani Clarence Seerdof ambaye aliifundisha klabu hiyo kwa miezi mitano .
    Aidha bodi ya utendaji ya klabu hiyo imewataja makocha wanaotazamiwa kupewa kibarua hicho ambao ni Jurgen Klopp,Vincenzo Montella na Luciano Spalletti.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: INZAGHI ACHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA AC MILAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top