RIPOTI ya rushwa ya FIFA iliyotolewa leo asubuhi imeisafisha Qatar kuandaa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022, lakini imeiweka shakani nafasi ya England kuandaa fainali za michuano hiyo mwaka 2018, ikisema kwamba walipata kura mbili tu.
Jaji wa maadili, Hans-Joachim Eckert aliyehusika katika uchunguzi wa uombaji wa uenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022 amehitimisha kwamba Qatar haikufanya dhambi yoyote ya kuwaponza wapokonywe uenyeji.
Lakini imeitia hatiani England kwa kutumia njia haramu, baada ya kukutwa na hatia ya kumshawishi na kumpa hongo Mjumbe wa zamani wa Kamati Kuu ya FIFA, Jack Warner. England ili kujisafishia njia ya kuandaa Kombe la Dunia 2018 wanadaiwa kumtumia Warner, waliandaa hafla ya chakula cha usiku ya Umoja wa Soka Caribbean, kuipa kambi ya mazoezi timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Trinidad, na kumpa Warner ofa ya kusaidia kituo chake cha Joe Public Football Team.
Qatar ilitajwa kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia 2022 na Rais wa FIFA, Sepp Blatter mwaka 2010
0 comments:
Post a Comment