• HABARI MPYA

    Thursday, November 13, 2014

    SUNZU AZUA HOFU ZAMBIA BAADA YA 'KUJERUHIWA' ULAYA

    Na Mwandishi Wetu, LUSAKA
    NAHODHA wa Zambia, Stopilla Sunzu (pichani kulia) ameenguliwa kwenye kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi zijazo za kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2015.
    Beki huyo wa timu ya daraja la kwanza Ufaransa, Sochaux anasumbiliwa na maumivu ya nyama aliyoyapata kwenye mechi ya Ligue 2, Novemba 7 baada ya kutolewa dakika ya 65 timu yake ikishinda 2-1 nyumbani dhidi ya Ajaccio.
    Daktari wa timu ya taifa ta Zambia, Joseph Kabungo amesema beki huyo amesafiri kwenda Lusaka kwa matibabu kuangalia uwezekano wa kupona.
    “Hatupingani na klabu yake juu ya walichomfanyia. Tunakubaliana nayo, lakini Stopilla si mchezaji wa Sochaux pekee, pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Zambia na wote tunaguswa naye,".
    Kukosekana kwa Sunzu ni pigo kubwa kwa safu ya ulinzi ya Zambia na kocha Honour Janza atalazimika kumtumia beki wa Nkana, Christopher Munthali acheze pamoja na Nyambe Mulenga wa Zesco United katika beki ya kati.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUNZU AZUA HOFU ZAMBIA BAADA YA 'KUJERUHIWA' ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top