• HABARI MPYA

    Wednesday, October 15, 2014

    RONALDO AING'ARISHA URENO KUFUZU EURO, MABINGWA WA DUNIA UJERUMANI WANG'ANG'ANIWA NYUMBANI

    BAO pekee la mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo scored dakika za majeruhi, limeipa Ureno ushindi wa 1-0 dhidi ya Denmark katika mechi ya I kufuzu Euro 2016 usiku wa jana.
    Ronaldo alifunga bao hilo akiunganisha krosi ya Ricardo Quaresma na kumtungua kipa Kasper Schmeichel kuipa timu yake pointi tatu dakika ya 95.
    Mechi nyingine za kundi hilo, baina ya wenyeji Serbia na Albania ilivunjika dakika ya 35 baada ya vurugu.  Kundi D, Ujerumani ikiwa nyumbani, imelazimishwa sare ya 1-1 na Iceland bao la akifunga Toni Kroos dakika ya 71 kabla ya John O'Shea kuwasawazishia wageni dakika ya 90.  
    Georgia imeifunga 3-0 Gibraltar na Poland imetoka 2-2 na Scotland. Kundi E Uswisi imeifunga 4-0 San Marino. Kundi F Hungary imeifunga 1-0 Faroe Islands, Romania imeifunga 2-0 Finland na Ireland Kaskazini imeifunga 2-0 Ugiriki.
    Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Ureno dhidi ya Denmark
    The Real Madrid forward started despite injury fears after being seen with an ice pack on his knee against France on Friday
    The Real Madrid forward started despite injury fears after being seen with an ice pack on his knee against France on Friday
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO AING'ARISHA URENO KUFUZU EURO, MABINGWA WA DUNIA UJERUMANI WANG'ANG'ANIWA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top