MKONGWE Didier Drogba ameshindwa kung'ara akiichezea Chelsea kwa mara ya kwanza tangu arejee msimu baada ya kuchapwa mabao 3-0 Werder Bremen nchini Ujerumani katika mchezo wa kujiandaa na msimu.
Mshambuliaji huyo wa Ivory Coast, aliichezea kwa mara ya mwisho Chelsea mwaka 2012 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikishinda kwa penalti dhidi ya Bayern Munich, lakini leo akirejea Ujerumani yeye na washambuliaji wengine wa The Blues- walilala kwa mabao ya Ludovic Obraniak kwa kichwa na penalti za Assani Lukimya na Felix Kroos.
Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois amefungwa mabao mawili leo, wakati bao lingine alifungwa Petr Cech kipindi cha pili
0 comments:
Post a Comment