YANGA SC imetangaza kumsajili kiungo mchezeshaji wa Ruvu Shooting ya Pwani, Hassan Dilunga ambaye kwa sasa yupo katika kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Diunga amefuzu kuingia kwenye kikosi cha wachezaji 32 wa Stars baada ya kufanya vizuri katika timu ya pili ya taifa, Future Young Taifa Stars iliyoundwa na kocha Mdenmark, Kim Poulsen kusaka wachezaji wa kupandisha timu ya kwanza, Taifa Stars.
Na baada ya kufanya vizuri katika mchezo wa kirafiki baina ya Future na Taifa Stars, ambayo timu ya pili iliwafunga kaka zao 1-0, Dilunga amepanda timu ya wakubwa.
Ni mchezaji mzuri, kiungo halisi anayejua kuchezesha timu, ingawa tu ana mambo mengi sana ambayo mengine hayaisaidii timu, zaidi huiathiri kwa namna moja au nyingine.
Ni fundi, anajua kuuchezea mpira ana vitu ambavyo mwanasoka yoyote anayeitwa mzuri angependa kuwa navyo, lakini ana tatizo sawa na la Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wa Azam, wanapenda kukaa na mpira kufanya madoido na hivyo kuichelewesha timu kushambulia na pia kuihatarisha kufungwa wanapopokonywa mpira na kutengenezwa shambulizi la ghafla na wapinzani.
Haya ni mambo ambayo mwalimu yeyote mzuri anaweza kuyafanyia kazi na Dilunga akacheza kwa manufaa ya timu. Niseme tu, binafsi nampenda sana huyo kijana tangu mwaka jana nilipoanza kumfuatilia baada ya kugundua kipajii chake.
Ni kama ilivyo tu kwa sahiba yangu Sure Boy, ambaye huwa nafanya kazi sana ya kumshauri abadilike kiuchezaji na kuachana na mchezo wa ‘anao anao’, badala yake atumie kipaji chake kutengeneza mashambulizi na hiyo ndiyo sifa kubwa ya kiungo mchezeshaji.
Sasa Dilunga atahamia Yanga, kama kweli amesaini huko kama ambavyo Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo, Abdalah Ahmed Bin Kleb amekaririwa na tovuti ya klabu hiyo akisema.
Kwa sasa Dilunga akiwa katika kambi ya Stars inayojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kenya keshokutwa, sitarajii kama hata atavaa jezi, kwa sababu nafasi yake ina wachezaji wengi wazuri na wazoefu.
Yupo Mwinyi Kazimoto na Salum Abubakar wote hawa Stars hutumika kama wachezeshaji na hupokezana, lakini pia Athumani Iddi ‘Chuji’ mara nyingine amekuwa akitumika katika nafasi hiyo, kwa kuwa Frank Domayo katika timu ya Kim Poulsen huchezeshwa kama kiungo mkabaji.
Kwa vyovyote, kwa ubora Dilunga anakuwa chaguo la tatu katika nafasi ya kiungo mchezeshaji Stars, baada ya Sure Boy na Mwinyi- maana yake hata kuvaa jezi Jumanne itakuwa bahati sana kwake.
Lakini unaweza kuona kama huyu kijana ni hazina ya taifa katika nafasi hiyo na anahitaji mwendelezo mzuri ili siku moja arithi mikoba ya akina Mwinyi na Sure Boy pale Stars.
Sasa yuko njiani kwenda Yanga SC, tujiulize huko atapata huo mwendelezo mzuri ili ndoto za yeye kuja kuwa tegemeo la taifa zitimie siku moja? Shaka tupu.
Yanga ina viungo sita, ambao wanacheza nafasi zote, chini na juu, inategemea na mfumo ambao kocha Mholanzi, Ernie Brandts anataka kuutumia katika mchezo husika.
Hao ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Salum Telela, Hamisi Thabit, Haruna Niyonzima, Frank Domayo na Nizar Khalfan, maana yake Dilunga anakwenda kuwa kiungo wa saba.
Kwa msimu huu, Brandts amekuwa akiwatumia Domayo na Chuji katikati, wakati wengine wamekuwa wakihamishwa nafasi na zaidi kuchezeshwa pembeni, ambako tayari kuna wachezaji wazuri wenye kasi kama Mrisho Ngassa na Simon Msuva. Kuna yule chipukizi aliyepandishwa kutoka Yanga B, Abdallah Mguhi ‘Messi’ pia.
Yanga ina wachezaji wazuri wa kiungo na ushambuliaji, hadi unaweza kuona inamshinda Brandts kuipanga. Hussein Javu amesajiliwa msimu huu kwa mamilioni lakini hadi sasa hajatumika ipasavyo. Brandts kuna wakati anawapanga pembeni washambuliaji Said Bahanuzi na Hamisi Kiiza, wakati timu ina viungo kibao, ndiyo maana nasema Yanga ina wachezaji wazuri wengi wa nafasi za kiungo na ushambuliaji hadi inamshinda Mholanzi huyo.
Lakini ukitazama haswa viungo wote waliopo Yanga, wote wana uwezo zaidi wa kucheza juu kuliko chini na unaweza kuona kabisa baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, kama ilivyo kwa Azam FC, Yanga pia wanahitaji kiungo mkabaji mzuri.
Lakini kabla ya kufikiria kuwa na kiungo mpya, Yanga inaweza kumtumia Mbuyu Twite katika nafasi ya kiungo mkabaji na Juma Abdul akaendelea kucheza nafasi ambayo ilifanya klabu hiyo ilimsajili, beki wa kulia.
Kulingana na ukweli huu, au hali halisi ndani ya Yanga, huwezi kuona sababu za msingi za klabu hiyo kumsajili Dilunga, labda tu kwa sababu ni mchezaji mzuri. Lakini inakuwaje ununue kiatu kizuri hata kama hakikutoshi?
Kila mchezaji ana bahati yake, Dilunga anaweza kufika Yanga akapendwa na kocha, akapewa nafasi, akafanya vizuri na kuendeleza kipaji chake. Lakini hapo tumezungumzia bahati, maana yake anakwenda kujaribu bahati yake Yanga.
Asipofanikiwa sasa, hatari yake ni kwamba, Simba na Yanga huwa hawajui kuwavutia subira wachezaji, hivyo mwakani anaweza kutolewa kwa mkopo kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Nahodha wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Omega Seme na wachezaji wengine wengi tu wazuri.
Tumuombee heri, ila kama kweli amesaini Yanga maana yake ‘amejilipua’, yaani amejitoa mhanga, liwalo na liwe. Lakini pamoja na hayo tujiulize, Yanga inasajili wachezaji inayowahitaji, au inasajili wachezaji wazuri hata kama haiwahitaji?

.png)
0 comments:
Post a Comment