• HABARI MPYA

    Wednesday, November 13, 2013

    SIMBA SC YAMSAJILI MDOGO WAKE MSUVA

    Na Mahmoud Zubeiry, Kariakoo
    MFUNGAJI bora wa mashindano ya Umoja na Amani, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ubungo Msewe, Dar es Salaam, James Msuva amesajiliwa timu ya vijana ya Simba SC, maarufu kama Simba B na tayari amejiunga nayo.
    Mhitimu huyo wa kidato cha Nne katika sekondari ya Makongo, Dar es Salaam aling’ara katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Waziri a Habari, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara akiichezea Baruti FC mwezi uliopita kwa kufunga mabao saba na kuiwezesha timu yake ya mtaani kutwaa Kombe hilo.
    Nani Mtani Jembe? James Msuva kulia akiwa na kaka yake Simon jana

    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana katika hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo, Dar es Salaam, Msuva alisema kwamba tayari amejiunga na Simba B chini ya kocha Suleiman Matola na amekwishaichezea mechi mbili za Ligi ya Vijana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kufunga bao moja. 
    James aliyekwenda Sapphire jana kumtembelea kaka yake, Simon Msuva wa Yanga SC aliye kambini na timu ya pili ya taifa, Future Young Taifa Stars, alisema kwamba anamshukuru Mungu anaendelea vizuri Simba B.
    “Natarajia kuichezea Simba katika mashindano ya Kombe la Uhai (michuano maalum ya timu za vijana za Ligi Kuu) na nikipata nafasi hiyo itakuwa fursa nzuri kwangu kuzidi kupambanua kipaji changu,”alisema.
    Msuva mdogo aliitwa na Waziri Mukangara ofisini kwake kwa lengo la kumsaidia zaidi kumuendeleza kisoka, baada ya kuonyesha kipaji kikubwa katika michuano ya Kombe la Umoja na Amani.
    Baba mmoja, mama mmoja lakini timu tofauti; James kulia na Simon kushoto

    “Nilikwenda kwa Mheshimiwa Waziri, tulizungumza, alinipa zawadi na kunihamasisha niongeze juhudi,”alisema James mwenye umri wa miaka 16, aliyefunga mabao yote mawili Baruti FC ikishinda 2-0 na kutwaa Kombe la Dk Fenella. 
    James anayemfuatia Simon Msuva kuzaliwa, amehitimu Kidato cha Nne katika sekondari ya Makongo, Dar es Salaam na pamoja na kuchezea Barudi FC kama timu ya mtaani, pia alikuwa katika akademi ya Wakati ya Ujao, iliyoasisiwa na kocha wa zamani wa Simba, Mholanzi Ronny Mintjens. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAMSAJILI MDOGO WAKE MSUVA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top