Na Ibrahim Kyaruzi, Dar es Salaam
MASHINDANO ya 12 ya mbio za Kilimanjaro Marathon yanayotarajiwa kufanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Machi 2, mwakani yamezinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Kavishe alisema anatarajia kwamba zawadi hizo za fedha zitawavutia wanariadha
mashuhuri na kuwapa moyo wengine kuvunja rekodi za mashindano hayo.
MASHINDANO ya 12 ya mbio za Kilimanjaro Marathon yanayotarajiwa kufanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Machi 2, mwakani yamezinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema:
“Ninayo furaha kutangaza kwamba huu utakuwa mwaka wa 12 kwa mbio za Kilimanjaro
Marathon kufanyika chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager.
Kwa mara nyingine, ni fahari kubwa kwa Kilimanjaro Premium Lager
kudhamini tukio hili maarufu na lenye msisimko mkubwa katika kalenda ya michezo
ya Tanzania.”
Kavishe alitangaza nyongeza ya asilimia 25 kwenye zawadi za fedha kwa washindi
wa mbio za kilometa 42 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, ambapo jumla ya zawadi
ya fedha itaongezeka kutoka Tsh milioni 15 hadi Tsh milioni 20, huku washindi
wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaume kwa wanawake wakipokea jumla ya Tsh milioni
nane na kiasi kilichobaki kikigawanywa miongoni mwa washindi wanne hadi wa 10.
Kavishe alisema kwamba ni bahati kubwa kwa Kilimanjaro Premium Lager kudhamini
mashindano haya yenye msisimko mkubwa katika kalenda ya michezo nchini Tanzania
na kwamba Bia ya Kilimanjaro Premium Lager itatoa zawadi kubwa za fedha kwa wanariadha
wakati wengine watabaki wana kumbukumbu isiyofutika ya ukaribu wa hali yajuu.
Ili kuwahamasisha na kuwapa motisha wanariadha wa Tanzania kuongeza viwango
vyao na kutumia muda mfupi kumaliza mbio hizo, Kilimanjaro Premium Lager imetenga
Shilingi milioni mbili kama bonasi au malipo ya nyongeza kwa wanariadha wa
Tanzania watakaovunja rekodi kwenye mashindano hayo.
Zawadi zitakazotolewa kwenye 2014 Kilimanjaro Marathon zimenyumbulishwa
kitakwimu kama ifuatavyo hapa chini;
2014
KILI MARATHON PRIZES
|
2013
KILI MARATHON PRIZES
| ||||
MALE
|
FEMALE
|
MALE
|
FEMALE
| ||
1ST
|
4,000,000
|
4,000,000
|
1ST
|
3,000,000
|
3,000,000
|
2ND
|
2,000,000
|
2,000,000
|
2ND
|
1,500,000
|
1,500,000
|
3RD
|
1,000,000
|
1,000,000
|
3RD
|
850,000
|
850,000
|
4TH
|
900,000
|
900,000
|
4TH
|
650,000
|
650,000
|
5TH
|
600,000
|
600,000
|
5TH
|
500,000
|
500,000
|
6TH
|
400,000
|
400,000
|
6TH
|
350,000
|
350,000
|
7TH
|
350,000
|
350,000
|
7TH
|
250,000
|
250,000
|
8TH
|
300,000
|
300,000
|
8TH
|
200,000
|
200,000
|
9TH
|
250,000
|
250,000
|
9TH
|
150,000
|
150,000
|
10TH
|
200,000
|
200,000
|
10TH
|
100,000
|
100,000
|
SUB
TOTAL
|
10,000,000
|
10,000,000
|
SUB
TOTAL
|
7,550,000
|
7,550,000
|
GRAND
TOTAL
|
20,000,000
|
GRAND
TOTAL
|
15,100,000
| ||
![]() |
| Bendera juu; Ole Gabriel na Nyambui kulia |
![]() |
| Mkurugenzi wa Masoko Vodacom, Kevin Twisa akihutubia katika hafla hiyo |
![]() |
| Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akihutubia |
![]() |
| Mjadala; Kutoka kulia Kevin Twisa, Mama Juliana Yassoda kutoka Wizara ya Habari na Salum Mwalimu |
![]() |
| Nyambui akihutubia |
![]() |
| Ole Gabriel akihutubia |
![]() |
| Kikundi cha sanaa cha THT kikiwasilisha bendera kwa mbwembwe za kisanii |
![]() |
| Nyambui akifurahia jambo na Ofisa wa Executive, Michael Mukunza kulia |
![]() |
| Mama Yassoda akimkabidhi cheti, Ibrahim Kyaruzi wa Executive Solutions kutambua mchango wa kampuni hiyo katika historia ya mbio hizo za kimataifa |
Aliongeza kwamba Kilimanjaro Marathon imepiga hatua kutoka tukio la
mkoa hadi kuwa mashindano makubwa ya kimataifa. “Tunatambuliwa na IAAF na Chama
cha Kimataifa cha Mbio za masafa Marefu. Licha ya mafanikio haya, tunaendelea kujitahidi
kuboresha mbio hizi mwaka hadi mwaka,” alisemaKavishe.
Tunashukuru kwa jinsi walivyoungwa mkono na Wizara ya Michezo na mamlaka
za Serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro, Riadha Tanzania, Chama cha Mbio za Ridhaa
Kilimanjaro, pamoja na wadhamini wenzawao ambao ni GAPCO, Simba Cement, CFAO
Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, FNB Bank na Kilimanjaro Water kwa
kusaidia kuikuza Kilimanjaro Marathon kuwa moja ya mashindano makubwa zaidi ya mbio
za masafa marefu barani Afrika.













.png)
0 comments:
Post a Comment