• HABARI MPYA

    Thursday, November 14, 2013

    ARSENAL YAPEWA OFA YA KUMSAJILI KALOU ALIYE MOTO ILE MBAYA UFARANSA HIVI SASA

    KLABU ya Arsenal imepewa ofa ya kumsajili Salomon Kalou ifikapo Januari.
    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea, kwa sasa anachezea klabu ya Lille ya Ufaransa, na yupo tayari kurejea Ligi Kuu England katika dirisha dogo.
    Na Kalou, anaweza kutolewa kwa dau la Pauni Milioni 2.5 amewaelekeza washauri wake kufutilia timu zinazomtaka England kuelekea Januari.
    Kiwango: Salomon Kalou ameifungia mabao 18  Lille tangu ajiunge nayo Julai 2012
    Blue: Juan Mata (top) congratulates Kalou after he scored for Chelsea against Benfica in the Champions League
    Bluu: Juan Mata (juu) akimpongea Kalou baada ya kuifungia bao Chelsea dhidi ya Benfica katika Ligi ya Mabingwa

    Arsenal ni miongoni mwa klabu ambazo zimekuwa zikimmezea mate nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast kwa wiki za karibuni.
    Na kama inavyofahamika The Gunners wapo sokoni kusaka mshambuliaji, basi milango iko wazi kwao.
    Kocha Arsene Wenger anataka kusajili mshambuliaji wa kusaidiana na mshambuliaji wake pekee wa sasa, Mfaransa Olivier Giroud, na bila shaka Kalou atafaa.
    Arsenal ilikaribia kumsajili Kalou Januari 2012, lakini mshambuliaji huyo alikataa baada ya kuambiwa atapunguziwa mshahara hadi Pauni 20,000 kwa wiki kutoka 60,000 alizokuwa akilipwa Stamford Bridge.
    Kocha wa West Bromwich, Steve Clarke pia alitaka kumsajili Kalou mwanzoni mwa msimu huu, lakini mchezaji mwenye kasi aliyezaliwa miaka 28 iliyopita akaamua kubaki Ufaransa.
    In need: Wenger (above) is in need of another striker at Arsenal
    Anahitaji: Wenger (juu) anahitaji mshambuliaji mwingine Arsenal
    No 1: Arsenal are in danger of being too reliant on star striker Olivier Giroud
    Namba 1: Arsenal iko hatarini kwa sababu ina mshambuliaji mmoja tu, Olivier Giroud ambaye akiumia klabu itabaki bila mshambuliaji
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAPEWA OFA YA KUMSAJILI KALOU ALIYE MOTO ILE MBAYA UFARANSA HIVI SASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top