• HABARI MPYA

  Friday, February 02, 2018

  HENRY AFUKUZWA WEST HAM KWA KUWABAGUA WAAFRIKA

  Tony Henry (kushoto) akiwa na kocha wa West Ham United, David Moyes mwanzoni mwa usajili wa Januari 


  NYOTA WA WEST HAM WENYE ASILI YA AFRIKA  

  West Ham ina wachezaji sita wa kikosi cha kwanza wenye asili ya Afrika. Wawili kati yao —Joao Mario na Angelo Ogbonna — wamechagua kuziwakilisha Ureno na Italia licha ya kwamba wazazi wao ni Waafrika. Pedro Obiang alichezea timu ya taifa za vijana ya Hispania lakini hajachezea timu ya wakubwa na bado ana nafasi ya kuiwakilisha Equatorial Guinea. Edimilson Fernandes anacheze Uswisi lakini ana asili ya Cape Verde. Beki wa kushoto, Arthur Masuaku bado hajaichezea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lakini aliitwaAgosti wakati Cheikhou Kouyate ni mchezji mzoefu wa kimataifa wa Senegal.
  Cheikhou Kouyate (Senegal) 
  Pedro Obiang (Equatorial Guinea)
  Joao Mario (Angola)  
  Angelo Ogbonna (Nigeria) 
  Arthur Masuaku (DRC) 
  Edimilson Fernandes (Cape Verde)
  KLABU ya West Ham imemfukuza Mkurugenzi wake wa Usajili, Tony Henry baada ya kutoa kauli tata juu ya wachezaji wa Kiafrika katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.
  Sportsmail ilifichua habari hiyo Jumatano usiku kwamba Henry ametuma barua pepe kwa mawakala wawili kuwaambia waache kupendekeza wachezaji wa Kiafrika katika timy yao. 
  Baadaye akasema ni kwa sababu wana tabia mbaya na wanasababisha ghasia wanapokuwa hawapo kwenye timu.
  Klabu hiyo ya Uwanja wa London ilimsimamisha Henry Alhamisi kabla ya kuamua kusitisha kibarua chake West Ham leo usiku. 
  Msemaji wa West Ham United amesema: "West Ham United leo imevunja mkataba na Mkurugenzi wa Usajili, Tony Henry mara moja kufuatia kauli zake zisizokubalika ambazo ziliripotiwa kwa mapana marefu kwenye vyombo vya habari,".
  "Hatua tuliyochukua imekuja baada ya uchunguzi kamili na wa kina. West Ham United haitavumilia aina yoyote ya ubaguzi,"imesema.
  Habari iliyoandikwa na Sportsmail ilisamabaa kwenye kikois cha West Ham jana. Kiungo Msenegal, Cheikhou Kouyate akaposti kwenye akaunti yake ya Instagram: 'Mwfrika na njivunia'.
  Posti yake hiyo ilipewa likes na Manuel Lanzini, Adrian, Pedro Obiang na Arthur Masuaku, wote wachezaji wa Kiafarika kwenye kikosi cha West Ham kwa sasa.KLABU ya West Ham imemfukuza Mkurugenzi wake wa Usajili, Tony Henry baada ya kutoa kauli tata juu ya wachezaji wa Kiafrika katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HENRY AFUKUZWA WEST HAM KWA KUWABAGUA WAAFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top