• HABARI MPYA

  Monday, January 09, 2017

  YANGA KUWAKOSA TAMBWE, NGOMA, ZULU NA CHIRWA KESHO DHIDI YA SIMBA

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  KOCHA wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba ataingia kwenye mchezo wa kesho dhidi ya mahasimu, Simba hali ya kikosi chake ikiwa si nzuri sana.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo, Lwandamina amesema kwamba wachezaji wake wanne tegemeo wote ni majeruhi na hawawezi kucheza kesho.
  Lwandamina aliwataja wachezaji majeruhi ni Wazambia wenzake, viungo Justin Zulu na Obrey Chirwa na washambuliaji Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma.
  George Lwandamina amesema wachezaji wake tegemeo wanne ni majeruhi kuelekea mchezo wa kesho

  Pamoja na hao, Lwandamina alisema beki Pato Ngonyani na mshambuliaji Matheo Anthony nao wote ni wagonjwa na hawana uhakika wa kucheza kesho.
  Kwa ujumla Lwandamina ambaye timu yake ilifungwa 4-0 na Azam FC Jumamosi kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A, alisema ataingia kwenye mchezo wa kesho katika mazingira magumu ya kukatisha tamaa.
  “Lakini hatuna namna nyingine, lazima tuingize timu tukapambane,”alisema. Yanga inakutana na mahasimu, Simba katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUWAKOSA TAMBWE, NGOMA, ZULU NA CHIRWA KESHO DHIDI YA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top