• HABARI MPYA

  Thursday, January 05, 2017

  SIMBA NA URA KATIKA BONGE LA MECHI LEO KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC inakamilisha mechi zake za Kundi A Kombe la Mapinduzi, kwa kumenyana na mabingwa watetezi, URA ya Uganda usiku wa leo.
  Mchezo huo utakaotanguliwa na mechi nyingine ya kundi hilo kati ya KVZ na Jang'ombe Boys kuanzia Saa 10:00 jioni, itaanza Saa 2:30 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Simba inayofundishwa na kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog itahitaji ushindi ili kuongoza kundi na kukwepa kukutana na wapinzani wa jadi, Yanga mapema.
  Lakini hilo litakuwa gumu mbele ya URA ambayo nayo itahitaji zaidi ushindi kwanza kujihakikishia tiketi ya Nusu Fainali.
  Simba inaongoza kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na URA, Taifa Jang’ombe na Jang’ombe Boys zenye pointi tatu kila mmoja.’
  Maana yake URA haina namna nyingine zaidi ya kushinda ili kuzipiku Taifa na Jang’ombe katika kinyang’anyiro cha tiketi ya Nusu Fainali.
  Simba kutaka ushindi na URA pia kutaka kushinda lazima kunamaanisha mechi yao leo ni nzuri.  
  Katika mechi ya Kundi B usiku wa jana, Azam FC ililazimishwa sare ya bila kufungana na Jamhuri ya Pemba Uwanja wa Amaan.
  Kwa sare hiyo, Azam inafikisha pointi nne na kuendelea kubaki nafasi ya pili nyuma ya Yanga, yenye pointi sita, ambayo jana jioni iliifunga Zimamoto 2-0.
  Azam sasa itacheza mechi yake ya mwisho Jumamosi dhidi ya Yanga, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati Zimamoto na Jamhuri. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA URA KATIKA BONGE LA MECHI LEO KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top