• HABARI MPYA

  Friday, January 13, 2017

  MAVUGO AANZIA BENCHI SIMBA NA AZAM LEO

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  KOCHA wa Simba SC, Mcameroon Joseph Marius Omog amemuanzishia benchi mshambuliaji Laudit Mavugo katika fainali ya Kombe la Mapinduzi inayoanza Saa 2:15 usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Omog amemuanzisha mshambuliaji mmoja tu, Juma Luizio mbele ya viungo Mwinyi Kazimoto, Muzamil Yassin, Jonas Mkude, Shiza Kichuya na James Kotei.
  Kwa ujumla kikosi cha Simba leo ni; Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Juma Luizio, Muzamiru Yassin na Mwinyi Kazimoto.
  Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Moris, Yakubu Mohammed, Stephan Mpondo, Joseph Mahundi, Salum Abubakar 'Sure Boy', John Bocco, Yahya Mohammed na Himid Mao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAVUGO AANZIA BENCHI SIMBA NA AZAM LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top