• HABARI MPYA

    Wednesday, January 18, 2017

    MALI NA MISRI HAKUNA MBABE, UGANDA YAANZA VIBAYA AFCON

    MZUNGUKO wa kwanza wa mechi za makundi Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017 umekamilishwa usiku w Jumanne kwa Mali na Misri kugawana pointi baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa Kundi D mjini Port-Gentil.
    Katika mchezo huo, Misri ilipata pigo dakika ya 13 baada ya kipa wake, Ahmed El Shenawy kuumia misuli katika jitihada za kuokoa krosi ya Moussa Marega.
    El Shenawy akashindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake ikachukuliwa mkongwe wa umri wa miaka 44, Essam El Hadary katikati ya kipindi cha kwanza, hivyo kuweka rekodi mpya ya mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kucheza AFCON.

    Vikosi vilikuwa; Mali: Oumar Sissoko, Ousmane Coulibaly, Salif Coulibaly, Molla Wague, Hamari Traore, Sambou Yatabare/Yves Bissouma dk65, Lassana Coulibaly/Samba Sow dk72, Yacouba Sylla, Mamoutou N’Diaye, Bakary Sako na Moussa Marega
    Misri: Ahmed El Shenawy/Essam El Hadary dk25, Ahmed Hegazy, Mohammed Abdel Shafi, Ali Gabr, Ahmed Fathi, Tarek Hamed, Mahmoud Hassan, Abdallah Said, Mohamed Elneny, Mohamed Salah/Ramadan Sobhi dk70 na Marwan Mohsen/Ahmed ‘Koka’ Hassan dk76.
    Mapema jioni katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo, bao pekee la mkwaju wa penalti la Andre Ayew dakika ya 33 liliipa Ghana ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda Uwanja wa Port-Gentil.
    Penalti hiyo ilitolewa baada ya Isaac Isinde kupoteza mpira na kumuangusha kwenye boksi Asamoah Gyan.
    Vikosi vilikuwa; Ghana: Brimah/Gyan Badu dk72, Partey, Twasam, J. Ayew/Acquah dk85, Wakaso, Rahman/Acheampong dk38, Amartey, Boye, Afful na A. Ayew.
    Uganda: Onyango, Ochaya, Kizito, Isinde/Serunkuma dk70, Mawejje, Kizoto/Shaban dk55, Massa, Iguma, Wasswa, Miya na Azira/Oloya dk46.
    Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi za pili za Kundi A, Gabon na Burkina Faso Saa 1:00 usiku na Cameroon na Guinea-Bissau kuanzia Saa 4:00 usiku zote Uwanja wa Stade d'Angondje.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALI NA MISRI HAKUNA MBABE, UGANDA YAANZA VIBAYA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top