• HABARI MPYA

  Tuesday, January 17, 2017

  DRC YAIPIGA MOROCCO, IVORY COAST YABANWA NA TOGO

  JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo jana imeibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Morocco katika mchezo wa Kundi C Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Stade d'Oyem nchini Gabon.
  Ahsante kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Junior Kabananga dakika ya 55 na DRC ikafanikiwa kulilinda bao hilo licha ya kumaliza mechi na wachezaji pungufu baada ya Joyce Lomalisa Mutambala kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 81.
  Junior Kabananga akikimbia kushangilia baada ya kuifungia DRC bao pekee dakika ya 55 

  Vikosi vilikuwa; DRC: Matampi; N'Sakala/Lomalisa dk65, Zakuani, Tisserand, Mpeko - Mubele, Mulumba, Bope, Mbemba, Kabananga/Maghoma dk72 na Bakambu/Mbokani dk77.
  Morocco: El Kajoui; Mendyl, Da Costa, Benatia, Dirar - El Kaddouri/En Nesyri dk61, Saiss/Fajr dk73, El Ahmadi, Boussoufa, Carcela/El Arabi dk79 na Bouhaddouz.
  Katika mchezo uliotangulia jioni ya jana, mabingwa watetezi Ivory Coast walilazimishwa sare ya bila kufungana na Togo Uwanja wa Stade d'Oyem.
  Pamoja na kupewa nafasi kubwa ya kushinda, Tembo wa Ivory Coast hawakuweza kufurukuta jana mbele ya Togo walioongozwa na Nahodha wao, Emmanuel Adebayor ambaye jana timu kwa sasa,
  Vikosi vilikuwal Ivory Coast: Gbohouo; Aurier, Bailly, Kanon, A.Traore; Serey Die, Seri/Doukoure dk65, Kessie; Zaha/Bony dk70, Kodjia/Gradel dk83 na Kalou.
  Togo: Agassa; Gakpe, Romao, Ouro-Akoriko, Djene; Dossevi/Agbegniadan dk87, F.Ayite, Atakora, Bebou; Laba/Akakpo dk82 na Adebayor/Boukari dk89.
  Michuano hiyo itaendelea leo kwa mechi za Kundi D, Ghana ikimenyana na Uganda ya beki wa Simba, Juuko Murshid na Uwanja wa Stade de Port Gentil kuanzia Saa 1:00 usiku kabla ya Misri kumenyana na Mali Saa 4:00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DRC YAIPIGA MOROCCO, IVORY COAST YABANWA NA TOGO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top