RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Giovanni Vincenzo 'Gianni' Infantino ameipongeza klabu ya Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2022-2023.
Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ikiwa na mechi mbili mkononi baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 74, saba zaidi ya wapinzani wao wakuu, Simba SC.
Na hilo linakuwa taji la 29 na la rekodi kwao baada ya awali, kubeba taji hilo katika misimu ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985,1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13, 2014–15, 2015–16, 2016–17 na 2021–2022.
wanafuatiwa na mahasimu, Simba amba wamechukua mara 22 katika misimu ya 1965, 1966, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1993, 1994, 1995, 2001, 2002, 2003, 2004, 2007, 2009–2010, 2011–2012, 2017–2018, 2018–2019, 2019–2020 na 2020–2021.
Timu nyingine zilizowahi kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania ni Cosmopolitans ya Dar es Salaam pia 1967, Mseto ya Morogoro 1975, Pan African ya Dar es Salaam pia 1982, Tukuyu Stars ya Mbeya 1986, Coastal Union ya Tanga 1988, Mtibwa Sugar ya Morogoro 1999 na 2000 na Azam FC msimu wa 2013–2014.
0 comments:
Post a Comment