• HABARI MPYA

  Friday, June 02, 2023

  INONGA NA MAYELE WAITWA KUIPIGANIA DRC IFUZU AFCON


  KOCHA Mfaransa, Sébastien Serge Louis Desabre wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amewajumuisha kikosini beki wa Simba Henock Inonga Baka na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Kalala Mayele kwa ajili ya mechi dhidi ya Gabon Juni 18.
  Chui wa DRC watakuwa wageni wa Gabón Juni 18 Uwanja wa Franceville Jijini Franceville katika mchezo wa Kundi I kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Ivory Coast.
  Hali ni mbaya kwa Desabre hadi sasa DRC ikiwa inashika mkia Kundi baada ya kuvuna pointi nne kwenye mechi nne, nyuma ya Mauritania yenye pointi tano, Sudan sita na Gabón saba - maana yake wanatakiwa kushinda meehi zote za mwisho kuangalia uwezekano wa kukata tiketi ya Ivory Coast mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: INONGA NA MAYELE WAITWA KUIPIGANIA DRC IFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top