// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RAIS SAMIA AWAALIKA YANGA SC IKULU KWA CHAKULA CHA MCHANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RAIS SAMIA AWAALIKA YANGA SC IKULU KWA CHAKULA CHA MCHANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, June 04, 2023

    RAIS SAMIA AWAALIKA YANGA SC IKULU KWA CHAKULA CHA MCHANA


    RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samiah Suluhu Hassan ameialika klabu ya Yanga kwa chakula cha jioni kesho Ikulu Jijini Dar es Salaam ikiwa ni pongezi zake kwao kwa kushika nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
    Rais Dk. Samia ameipongeza Yanga kwa mafanikio hayo na kusema;
    “Hongereni sana Yanga kwa hitimisho la mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup). Historia mliyoandika katika safari yenu ya michuano hii ni kubwa na ya heshima kwa Taifa letu. Nawatakia kheri katika mipango yenu ya siku zijazo,”.
    Yanga jana ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya USM Alger katika mchezo wa marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria.
    Lakini ni USM Alger waliofanikiwa kutwaa Kombe hilo kwa faida ya mabao ya ugenini kufuatia ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Jijini Dar es Salaam.
    Shirikisho Afrika licha ya kufungwa 1-0 na Yanga katika mchezo wa marudiano wa Fainali usiku huu
    USM Alger wamenufaika na ushindi wa ugenini wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza, kwani pamoja na sare ya jumla ya 2-2, lakini wamefaidika na mabao ya ugenini.
    Katika mchezo wa jana bao pekee la Yanga lilifungwa na beki wa kulia, Juma Shabani kwa penalti dakika ya saba baada ya Mzambia Kennedy Musonda kuangushwa kwenye boksi.
    Kipa wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra aliinusuru Yanga kuruhusu bao leo baada ya kupangua mkwaju wa penalti wa beki 
    Zinéddine Belaïd dakika ya 59 na baada ya mchezo akapewa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi.
    Mshambuliaji Fiston Kalala Mayele ameibuka Mfungaji Bora wa Kombe la Shirikisho kwa mabao yake saba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS SAMIA AWAALIKA YANGA SC IKULU KWA CHAKULA CHA MCHANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top