• HABARI MPYA

  Monday, June 05, 2023

  AL AHLY YAICHAPA WYDAD 2-1 CAIRO


  WENYEJI, Al Ahly SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa watetezi, Wydad Athletic Club katika Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika usiku huu Uwanja wa Kimataifa wa Cairo Jijini Cairo nchini Misri.
  Mabao ya Al Ahly yamefungwa na washambuliaji wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Percy Muzi Tau dakika ya 45 na ushei na Mahmoud Soliman ‘Kahraba’ dakika ya 59, wote wakimalizia pasi ya Hussein El Shahat.
   Bao pekee la Wydad limefungwa na mshambuliaji Mmorocco, Saif-Eddine Bouhra dakika ya 86 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Msenegal, Bouly Junior Sambou na timu hizo zitarudiana Juni 11 Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY YAICHAPA WYDAD 2-1 CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top