• HABARI MPYA

  Monday, June 05, 2023

  AUGUSTINE OKRAH APEWA MKONO WA KWAHERI SIMBA SC


  WINGA Mghana, Augustine Okrah amekuwa mchezaji wa kwanza kuruhusiwa kuondoka Simba wakati msimu unaelekea ukingoni.
  Taarifa ya Simba SC imesema; "Baada ya kuwa kwenye kikosi chetu kwa msimu mmoja, Augustine Okrah hatakuwa sehemu ya timu yetu ya msimu ujao,".
  Okrah alikuwa na mwanzo mzuri Simba baada ya kufunga bao la kuongoza Oktoba 23, mwaka jana katika sare ya 1-1 na watani, Yanga kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya NBC, kabla ya Mburkinabe Stephane Aziz Ki kuisawazishia Yanga dakika ya 45.
  Lakini baada ya hapo akaanza kuandamwa maumivu yaliyomiweka nje kwa sehemu kubwa ya msimu kabla ya kuanza kucheza mwezi uliopita.
   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AUGUSTINE OKRAH APEWA MKONO WA KWAHERI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top