• HABARI MPYA

  Monday, March 13, 2023

  KOCHA MPYA STARS AWACHUNIA MZIZE, KAPOMBE NA TSHABALALA


  KOCHA mpya wa timu ya taifa, Mualgeria, Adel Amrouche ameita wachezaji 31kuunda kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Uganda mwezi huu.
  Haya hivyo, kwenye kikosi hicho hajamjumuisha mshambuliaji chipukizi anayefanya vizuri kwa sasa, Clement Mzize wa Yanga, huku pia akiwaacha mabeki wa Simba, Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.
  Taifa Stars itaanzia ugenini Jijini Cairo nchini Misri kumenyana na Uganda Machi 24, kabla ya timu hizo kurudiana Jijini Dar es Salaam Machi 28.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA MPYA STARS AWACHUNIA MZIZE, KAPOMBE NA TSHABALALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top