• HABARI MPYA

    Tuesday, May 02, 2017

    SIMBA NA MBAO FAINALI KOMBE LA TFF UWANJA WA JAMHURI, DODOMA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    FAINALI ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayojulikana kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) itafanyika Mei 28, mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
    Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba Kanuni ya 5 ya michuano ya ASFC kuhusu Uwanja wa mashindano inasema: “Uwanja wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD utakuwa ni uwanja wenye hadhi inayokubalika na TFF,”.
    Na kwa sababu hiyo, Karia amesema kwamba kwa kuwa fainali ya mwaka huu itahusisha timu za mikoa tofauti, Simba ya Dar e Salaam na Mbao FC ya Mwanza, wameamua Uwanja wa Jamhuri utumike.
    Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia amesema akizungumza leo mjini Dar es Salaam 

    Fainali ya mwaka jana ilizikutanisha timu za Dar es Salaam tupu, Azam na Yanga iliyoibuka bingwa kwa ushindi wa 3-0 hivyo hakukuwa na droo ya kuchagua Uwanja.
    Tayari Yabga imevuliwa taji la ASFC, kufuatia kipigo cha 1-0 kutoka kwa wenyeji, Mbao FC katika mchezo wa Nusu Fainali jana jioni Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 
    Yanga wenyewe walijifunga bao hilo dakika ya 27, baada ya beki wake, Andrew Vincent ‘Dante’ kuunganishia nyavuni kwake krosi ya Pius Buswita katika harakati za kuokoa.
    Simba yenyewe iliitoa Azam FC katika Nusu Fainali ya kwanza Jumamosi Uwanja wa Taifa kwa ushindi wa 1-0 pia, bao pekee la Mohammed ‘Mo’ Ibrahim kipindi cha pili, mchezaji ambaye hata hivyo hakumaliza mchezo baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA MBAO FAINALI KOMBE LA TFF UWANJA WA JAMHURI, DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top