• HABARI MPYA

    Thursday, May 12, 2016

    KINDA WA AZAM FC AFUZU MAJRIBIO AMAZULU, LAKINI…

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO chipukizi wa Azam FC, Omar Wayne amefaulu majaribio katika klabu ya AmaZulu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, lakini kutokana na umri wake mdogo wa miaka 18 ameambiwa akaanzie timu B.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jana kutoka Durban, Wayne amesema kwamba AmaZulu wamemuambia akaanzie timu B ili apate uzoefu zaidi.
    Hata hivyo, Wayne amesema kwamba kwa kuwa timu B atakuwa amesaini Mkataba wa soka ya ridhaa hana uhakika kama Azam FC itamuachia bure.
    “Kwanza timu B maana yake hawa hawawezi kuilipa Azam, sasa na mimi nina Mkataba na Azam, sijui itakuwaje…ila nimewaambia sasa wakasema wanakwenda kufanya kikao, nasubiri majibu ya kikao chao,”alisema Wayne jana.
    Omar Wayne akiwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha AmaZulu jana
    Wayne ni mchezaji wa akademi ya Azam FC ambaye msimu huu alitolewa kwa mkopo Majimaji ya Songea ili akaanze kupata uzoefu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, Wayne alihamia Coastal Union pia kwa mkopo ambako wiki mbili zilizopita aliondoka kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio.
    Wakala Rogers wa Afrika Kusini alivutiwa na Wayne baada ya kumuona akiichezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Boys dhidi ya U17 ya Afrika Kusini mwaka jana.
    Pamoja na Serengeti kutolewa, lakini soka ya Wayne iliwavutia wengi na tangu hapo wamekuwa wakimfuatilia kabla ya kupewa nafasi ya majaribio ya kucheza Afrika Kusini.
    Wayne na Ibrahim Hajib wamekutana mjini Durban na wote wako chini ya Rodgers

    Mbali na Wayne, mchezaji mwingine wa Tanzania ambaye kwa sasa yupo kwenye majaribio Afrika Kusini ni mshambuliaji Ibrahim Hajib wa Simba ambaye leo anatarajiwa kuanza majaribio Golden Arrows pia ya Ligi Kuu ya nchi hiyo.
    Ni mchezaji mmoja tu ambaye inafahamika anacheza Ligi Kuu ya ABSA ya Afrika Kusini, Mrisho Khalfan Ngassa wa Free State Stars.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KINDA WA AZAM FC AFUZU MAJRIBIO AMAZULU, LAKINI… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top