• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 28, 2016

  YANGA SC NA CERCLE DE JOACHIM KATIKA PICHA JANA TAIFA

  Mshambuliaji wa Yanga SC, Amissi Tambwe akimuacha chini beki wa Cercle de Joachim katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0 na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya awali kushinda 1-0 Mauritius wiki mbili zilizopita
  Kiungo wa Yanga SC, Thabani Kamusoko akipasua katikati ya wachezaji wa Cercle de Joachim
  Winga wa Yanga SC, Simon Msuva akijaribu kumgeuza beki wa Cercle de Joachim
  Winga wa Yanga SC, Godfrey Mwashiuya (kulia) akitafuta maarifa ya kumpita beki wa Cercle de Joachim
  Mshambuliaji wa Yanga SC, Malimi Busungu akiwatoka mabeki wa Cercle de Joachim
  Amissi Tambwe akiwa juu kabisa kuwania mpira wa juu dhidi ya wachezaji wa Cercle de Joachim

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC NA CERCLE DE JOACHIM KATIKA PICHA JANA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top