• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 24, 2016

  CHEKA AMKATIA KILO NANE MZUNGU, KAZI IPO JUMAMOSI LEADERS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BONDIA Francis Cheka, amepunguza uzito wa kilogramu nane kutokana na mazoezi makali kujiandaa na pambano dhidi ya Muingereza mwenye asili ya Serbia, Geard Ajetoviv litakalofanyika Jumamosi kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar es Salaam kuwania ubingwa wa Mabara wa WBF uzito wa Super Middle. 
  Akizugumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana Cheka ambaye anaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Mango baada ya awali kuweka kambi ya wiki tatu Zambia, amesema kwamba alianza mazoezi chini ya kocha Saleh Abdallah akiwa ana uzito wa kilogramu 84, lakini sasa zimepungua hadi kubaki 76.
  Francis Cheka anaonekana yuko kabisa kwa pambano la Jumamosi

  “Nina kila sababu ya kuhakikisha nafanya vizuri kwenye mchezo huo, ni pambano kubwa nahitaji kushinda,”,alisema Cheka.
  Akizungumzia upande wa maandalizi kwa ujumla alisema yanaendelea vizuri kutokana na kwamba yuko kwenye hatua za mwisho za maandalizi ya pambano hilo. 
  Promota wa pambano hilo, Jumanne Msangi, alisema majaji na waamuzi wa pambano hilo, wanatarajia kawasili leo (Jumatano), tayari kwa pambano hilo. 
  Msangi alisema ugeni huo, utakapowasili nchini, moja kwa moja utakwenda kuonana na Waziri wa Habarani Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye ambaye anaamini watajadiliana kuhusiana na kupandisha mchezo wa ngumi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHEKA AMKATIA KILO NANE MZUNGU, KAZI IPO JUMAMOSI LEADERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top