• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 28, 2016

  CHEKA ATWAA UBINGWA WA WBF BAADA YA KUMSHINDA MZUNGU KWA POINTI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BONDIA Francis Cheka 'SMG' usiku wa kuamkia leo ametwaa ubingwa wa Mabara wa WBF uzito wa Super Middle baada ya kumshinda kwa pointi, mpinzani wake, Geard Ahevotic, Mserbia anayeishi Uingereza katika pambano la raundi 12 viwanja vya Leaders Club,, Dar es Salaam.
  Pambano hilo ambalo limehudhuriwa na mashabiki wengi wa mchezo huo, lilichelewa kuanza kutokana na kuwa hadi mida ya saa mbili usiku, walikuwa bado wakifunga ulingo wa kimataifa, ambao toka Serikali wakabidhiwe,Cheka anautumia kwa mara ya kwanza katika pambano lake la
  kimataifa.
  Pambano hilo ambalo limetaliwa na maneno mengi kutoka kwa baadhi ya mashabiki ambao walihudhuria mchezo huo, huku wengine wakishuhudia likirushwa live katika kituo cha Television ya Taifa TBC, na vituo vingine vya Luninga, lilitanguliwa na mapambano ya utangulizi, toka kwa mabondia wa uzito tofauti.
  Francis Cheka (kushoto) akimtandika ngumi ya mbavu Geard Ajevotic

  Katika pambano la Cheka ambalo liliamuliwa na mwamuzi toka WBF,majaji watatu, ambao walihusika kutoa ushindi mbele ya rais wa WBF, Howard Golberg, lilimpa ushindi Cheka, kutokana na utulivu alioonyesha akiwa ulingoni, tofauti na mpinzani wake Ajetovic.
  Katika pambano hilo ambalo Ajetovic, alipania kumpiga kwa
  KO,Cheka,jaji wa kwanza alitoa pointi 115,-112, huku wa pili akimpa 115,-112, na watatu alitoa 116 -111, ambazo zilitosha kutmpa ubingwa Cheka aliyefanikiwa kurusha ngumi nyingi ambazo hazikuwa na nguvu,
  lakini zilimpa pointi kutokana na kupiga sehemu husika.
  Kutokana na hilo Cheka alitangazwa mshindi wa pambano hilo, na kukabidhiwa mkanda huo na Susan Mungi kutoka TBC.
  Baada ya ushindi huo, Cheka alisema kwamba anamshkuru Mungu kwa ushindi alioupata, pamoja na kuwa amekutana na upinzani mkali kutoka kwa Ajetovic.
  Alisema Ajetovic amekuwa akitumia nguvu zaidi kurusha ngumi na kujikinga usoni, akisahau kutafuta pointi kwa kupiga sehemu zinazotakiwa.
  "Ajetovic alipania kunipiga kwa KO, lakini ilikuwa vigumu kwangu, kwa sababu nilijiandaa na ninamjua ni mzuri,"alisema Cheka.
  Alisema Ajetovic ana ngumi nzito, lakini hazina pointi katika mchezo kwa sababu alikuwa anapiga bila mpangilio.
  Hata hivyo Ajetovic, aligoma kuzungumza na waandishi wa habari, kwa kile alichokiona kuwa Cheka amependelewa na majaji waliohusika kutoa pointi kwa mpinzani wake.
  Katika pambano la utangulizi bondia Cosmas Cheka alimpiga Mustapha
  Dotto kwa pointi  na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa WBF Afrika, katika pambano la raundi 10, la uzito wa Light, likifuatiwa na pambano katika ya Mohamed Matumla, ambaye alimpiga Bakari Mohamed kwa pointi, katika
  pambano la raundi ya sita la uzito wa light weight, huku Seleman Zugo, akimshinda kwa pointi Mwinyi Mzengela, katika pambano la uzito wa Welter, raundi sita.
  Pambano lingine la utangulizi lilikuwa kati ya bondia Lulu Kayage, ambaye alichuana na Mwanne Haji, katika pambano la uzito wa Fly, raundi nne, huku Abdallah Pazi 'Dula Mbabe'alimpiga kwa KO, raundi ya nne,bondia Baraka Mwansope katika pambano la uzito wa kati raundi
  10,Mohamed Amir,akimpiga kwa pointi Yusuph Kombo, katika pambano la uzito wa Lightfly raundi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHEKA ATWAA UBINGWA WA WBF BAADA YA KUMSHINDA MZUNGU KWA POINTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top