• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 25, 2016

  NDONDI ZA RIDHAA WATAJA KIKOSI CHA OLIMPIKI, MABONDIA 18 WAPETA

  Nahodha Selemani Kidunda
  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), limeteuamabondia 18 kwa ajili ya timu ya taifa, itakayoshiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo ya kufuzu Olimpiki ya Rio, Brazil Agosti mwaka huu, yatakayofanyika mjini Yaounde,  Cameroon kuanzia Machi 9 hadi 20, mwaka huu.
  Makamu wa Rais wa BFT, Lukelo Anderson Willilo amewataja mabondia hao ni wa uzito wa Light Fly; Said Jabir wa Ngome na Mustafa Amri (Kawe, uzito wa Fly; Said Omary wa Kigoma na George Constantino wa Ngome.
  uzito wa Bantam; Hamadi Furahisha na Hamduni Issa wote wa JKT, uzito wa Light; Ismail Galiatano wa Ngome, Mwalami Salumu wa Temeke na Nasa Mafuru wa Magereza, uzito wa Light Welter; Kevin Kipinge wa Ngome na Adam Hassan wa JKT.
  Uzito wa Welter ni Nahodha Selemani Salum Kidunda wa Ngome, uzito wa Middle, Joseph Peter wa Ngome na Moses John  wa Kigoma, uzito wa Light Heavy; Leonard Machichi wa Ngome na Mohamed Hakimu wa Kawe uzito wa Heavy; Alex Sita Mpini Sulwa wa JKT na uzito wa Super Heavy; Haruna Swanga Mhando wa Ngome.
  Timu hiyo itakuwa chini ya kocha Mkenya Benjamin Musa Oyombi mwenye nyota tatu ya ukocha wa Kimataifa inayotambuliwa na shirikisho la Ngumi la Dunia (AIBA), ambaye atasaidiwa na Remmy Ngabo wa Magereza, Said Omary 'Gogopoa' wa Temeke na Jonas Mwakipesile.
  Wilillo amesema kwamba kwenye mashindano ya kufuzu Olimpiki yatakayofanyika Yaounde, Cameroon Machi 9 hadi 20, mwaka huu, timu ya Taifa itapeleka mabondia wanane.
  "Shirikisho liko katika mchakato wa kutafuta kiasi cha Dola za kimarekani 29,300 (Tzs 64,500,000), Tunaomba wadau, wadhamini na serikali kujitokeza kutuunga mkono kufanikisha safari hii kwenda kushiriki mashing a no haya ya kufuzu nchini Cameroon,"amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NDONDI ZA RIDHAA WATAJA KIKOSI CHA OLIMPIKI, MABONDIA 18 WAPETA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top