• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 21, 2016

  KAMUSOKO ALIKUWA KIBOKO KWA KUWAGONGA WACHEZAJI WA SIMBA JANA

  TAKWIMU ZA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA
  Yanga Simba 
  Mipira ya kurusha 22 14
  Rafu 21 14
  Kadi za njano 2 1
  Kadi nyekundu 0 1
  Kona 8 1
  Mashuti yaliyolenga lango 2 3
  Mashuti nje ya lango 2 8
  Kuotea 5 1
  Kubebwa na machela 2 0
  Thabani Kamusoko (kushoto) jana aliongoza kwa kuwachezea rafu wachezaji wa Simba

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Mzimbabwe wa Yanga, Thabani Scara Kamusoko jana alitia fora kwa kucheza rafu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, timu yake ikiilaza 2-0 Simba.
  Yanga SC walicheza jumla ya rafu 21, huku Kamausoko akiongoza kwa kucheza faulo mara tano - na Simba walicheza rafu mara 14, huku beki wake wa kulia, Hassan Kessy akiongoza kwa kucheza rafu nne.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba SC walipata kona nane, lakini zote hazikuwasaidia kupata bao, wakati mahasimu wao, Yanga SC walipata kona moja tu, tena mwishoni mwa mchezo. Kona zote za Simba zilikuwa zinapigwa na beki Hassan Kessy, wakati moja tu alipiga Ibrahim Hajib, wakati ya Yanga ilipigwa na Simon Msuva dakika ya 90.
  Katika kuwatibulia wapinzani, Simba SC pia walikuwa vizuri zaidi, wakitoa mipira 22, wakati Yanga walitoa mara 14. 
  Yanga walipata kadi mbili tu za njazo, ambazo walionyeshwa mfungaji wa bao la pili, Amissi Tambwe dakika 69 kwa kujiangusha na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’dakika ya 89 kwa kupoteza muda, huku Simba wailambwa kadi za njano mbili, zote akionyeshwa beki wake wa kati, Abdi Banda dakika ya 20 na 24 alipotolewa kwa kadi nyekundu.
  Simba SC walipiga mashuti matatu tu yaliyolenga lango kupitia kwa Jonas Mkude dakika ya 15, Hamisi Kiiza dakika ya 49 na Danny Lyanga dakika ya 93, wakati mashuti nane yalikwenda nje, kati ya hayo kiungo Said Ndemla pekee akipiga matatu na mshambuliaji Ibrahim Hajib mawili, mengine Lyanga na beki Juuko Murshid.
  Upande wa Yanga SC, mashuti ukiondoa mabao mawili waliyofunga, walilenga mashuti matatu langoni ambayo hayakuzaa mabao kupitia kwa Thabani Kamusoko dakika ya 14 na Simon Msuva mara mbili dakika za 76 na 82. 
  Yanga waliotea mara tano, Ngoma pekee akiotea mara 4 na Haruna Niyonzima mara moja, wakati Simba wao walioteamara moja tu kupitia kwa Kiiza
  Watu wa huduma ya kwanza waliingia uwanja mara mbili kuwabeba kwenye machela wachezaji wa Yanga, kiungo Deus Kaseke dakika ya 59, baada ya kugongana na Hassan Kessy ambaye haakurejea na nafasi yake ikachukuliwa na Simon Msuva na Ngoma dakika ya 71, baada ya kugongana na Juuko Murshid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAMUSOKO ALIKUWA KIBOKO KWA KUWAGONGA WACHEZAJI WA SIMBA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top