• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 21, 2016

  MTOTO WA KABUNDA ATUPIA ZOTE MBILI MWADUI YAICHAPA COASTAL 2-1, MTIBWA YAANGUKIA UGOKO SONGEA

  MATOKEO YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Leo Februari 21, 2016
  Majimaji 1-0 Mtibwa Sugar
  Ndanda FC 2-1 African Sport
  Mwadui FC 2-1 Coastal Union
  Jana Februari 20, 2016
  Yanga SC 2-0 Simba SC
  Mgambo JKT 1-1 Prisons
  Stand United 1-1 JKT Ruvu
  Mbeya City 0-3 Azam FC
  Toto Africans 1-1 Kagera Sugar


  MSHAMBULIAJI kinda, Hassan Salum Kabunda (pichani kulia), mtoto wa beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Salum Kabunda 'Ninja' amefunga mabao yote mawili, Mwadui FC ikishinda 2-1 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Mtoto huyo wa beki wa zamani wa Yanga na Tukuyu Stars, marehemu Kabunda 'Ninja Msudan' alifunga mabao hayo dakika ya 27 na 34, wakati la Coastal limefungwa na Hamadi Juma dakika ya 57.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Majimaji imeifunga 1-0 Mtibwa Sugar Uwanja wa Majimaji mjini Songea na Ndanda imeifunga 2-1 African Sports Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. 
  Ilibaki kidogo tu mchezo huo uishe kwa sare ya 1-1, Ndanda wakitanguliwa kupata kupitia kwa Omar Mponda dakika ya 45 kwa penalti kabla ya Sports kusawazisha kwa penalti pia kupitia kwa Ally Ramadhani dakika ya 79.
  Lakini Nahodha Kiggi Makassy akaifungia Ndanda bao la ushindi dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika za kawaida na kuwainua kwa furaha mashabiki wa nyumbani.
  Majimaji inafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 20 na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 15, Mtibwa Sugar ikibaki nafasi ya nne na pointi zake 33 za mechi 19, wakati Mwadui inafikisha pointi 32 baada ya kucheza mechi 20 na kupanda hadi nafasi ya tano kutoka ya saba na Coastal inabaki nafasi ya 13 na pointi zake 16 za mechi 20 pia. 
  Ndanda inafikisha pointi 23 baada ya kucheza mechi 20 na kupanda hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu kutoka ya 10, huku African Sports ikibaki na pointi zake 16 baada ya kucheza jumla ya mechi 20 sasa na kuteremka hadi nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTOTO WA KABUNDA ATUPIA ZOTE MBILI MWADUI YAICHAPA COASTAL 2-1, MTIBWA YAANGUKIA UGOKO SONGEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top