• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 21, 2016

  SAMATTA AONGEZEWA DAKIKA KRC GENK IKILAZIMISHA SARE YA 0-0 UGENINI UBELGIJI

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta (pichani kulia) jana ameongezewa dakika za kucheza katika klabu yake mpya, KRC Genk ikilazimisha sare ya 0-0 ugenini dhidi ya wenyeji Lokeren katika Ligi Kuu ya Ubelgiji, maarufu kama Pro League.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa 
  Daknam mjini Lokeren, Samatta aliyesajiliwa Januari kutoka TP Mazembe ya DRC aliingia dakika ya 60 kuchukua nafasi ya Mgiriki, Nikolaos Karelis.
  Na hiyo ilikuwa mara ya tatu mfululizo, Samatta anatokea benchi kwenda kuchukua nafasi ya Karelis, aliyesajiliwa pia Januari kutoka Panathinaikos ya kwao.
  Katika mechi ya ugenini dhidi ya Mouscron-Peruwelz, Genk ikishiinda 1-0, huo ukiwa mchezo wa kwanza kabisa wa Samatta Pro League Februari 6, 2016, Mtanzania huyo aliingia dakika ya 73 kumpokea Karelis.
  Mchezo wa Jumamosi iliyopita, Februari 13 Genk ikishinda 6-1 dhidi ya Waasland-Beveren Uwanja wa Cristal Arena mjini Genk, Samatta alimpokea Karelis pia dakika ya 73.
  Na baada ya kazi nzuri katika mechi hizo mbili za kwanza, kocha Mbelgiji mwenye umri wa miaka 51, Peter Maes akamuongezea muda wa kuwa uwanjani Samatta kwa dakika 13 zaidi – yaani kutoka kucheza dakika 17 mara mbili mfululizo hadi kucheza dakika 30.
  Genk inatarajiwa kushuka tena dimbani Jumapili ijayo ijayo nyumbani kumenyana na Club Brugge katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AONGEZEWA DAKIKA KRC GENK IKILAZIMISHA SARE YA 0-0 UGENINI UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top