• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 24, 2016

  AZAM YASHINDWA KUITOA YANGA KILELENI, YAKABWA NA PRISONS, SARE 0-0 LIGI KUU

  AZAM FC imeshindwa kuwaengua kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mabingwa watetezi, Yanga baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji Prisons jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Prisons ambayo pia iliipunguza kasi Yanga SC kwa kutoa nayo sare ya 2-2 mapema mwezi huu mjini humo, leo ilionekana kucheza tena kwa tahadhari kuepuka kufungwa.
  Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ijiongezee pointi moja na kufikisha 46 sawa na Yanga SC baada ya timu zote hizo kucheza mechi 19, lakini mabingwa watetezi wanaendelea kukamata usukani kwa wastani wao mzuri wa mabao.

  Simba SC wanaendelea kukamata nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, kwa pointi zao 45 za mechi 20.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, David Mwantika, Ramadhani Singano ‘Messi’, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Jean Baptiste Mugiraneza, Kipre Bolou/Farid Mussa dk63, John Bocco/Allan Wanga dk88 na Kipre Tchetche.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM YASHINDWA KUITOA YANGA KILELENI, YAKABWA NA PRISONS, SARE 0-0 LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top