• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 29, 2016

  SIMBA SC YAMSIMAMISHA NAHODHA KWA 'KUMTUKANA' KOCHA MAYANJA JANA TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba ya Dar es Salaam imemsimamisha Nahodha wake Msaidizi, Hassan Isihaka (pichani kulia) kwa muda usiojulikana kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.
  Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Manara kwa BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo imesema kwamba hatua hiyo imefikiwa baada ya mchezaji huyo kumtolea 'maneno machafu' kocha wa Simba, Mganda Jackson Mayanja.
  Manara amesema Isihaka ambaye pia ni beki wa kati wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars alifanya kitendo hicho kabla ya mechi ya jana ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Singida United Uwanja wa Taifa, Dar es Salmaa.
  Inadaiwa Isihaka alimtukana Mayanja kwenye chumba cha kubadilishia nguo Uwanja wa Taifa kabla ya mchezo huo wa michuano ya Kombe la Azam Sports Federation ambao SImba ilishinda 5-1. 
  "Kutokana na kitendo hicho kisicho cha kiungwana kilichofanywa mbele ya wachezaji wenzake na kinachokiuka waraka wa maadili(code of conduct) Kamati ya utendaji licha ya kumsimamisha mchezaji huyo, pia imeagiza alipwe nusu mshahara katika kipindi chote cha adhabu yake,"imesema taarifa ya Manara.
  "Pia kamati hiyo imewataka wachezaji wote kuzingatia nidhamu na weledi katika kipindi chote wanapoitumikia klabu ya Simba,"
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMSIMAMISHA NAHODHA KWA 'KUMTUKANA' KOCHA MAYANJA JANA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top