• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 28, 2016

  YANGA WAENDA PEMBA ‘FASTA’ KUSAKA UBANI WA KUILEWESHA AZAM FC JUMAMOSI TAIFA

  TATU BORA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
                           P W D L GF GA GD Pts
  Yanga 19 14 4 1 44 9 35 46
  Azam FC         19 14 4 1 34 11 23 46
  Simba SC 20 14 3 3 35 13 22 45 

  Yanga inapanda ndege kwenda kisiwani Pemba kesho kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Jumamosi ijayo

  BAADA ya ushindi wa 2-0 jana dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga inapanda ndege kwenda kisiwani Pemba kesho kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Jumamosi ijayo.
  Yanga imesonga mbele, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afriuka kwa kuitoa kwa jumla ya mabao 3-0 Cercle de Joachim baada ya awali kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita Mauritius.
  Sasa mabingwa hao watetezi wanarudi kwenye vita ya Ligi Kuu, Machi 5 wakimenyana na washindani wao wakuu katika mbio za taji, Azam FC.
  Zote, Yanga na Azam FC zina pointi 46 baada ya kucheza mechi 19 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara – lakini mabingwa watetezi wapo kileleni kwa wastani mzuri wa mabao (GD).
  Mchezo wa Jumamosi umebeba taswira halisi ya nani atajiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa msimu huu na timu zote zimewekeza katika maandalizi mazuri ndani na nje ya Uwanja.
  Azam FC wanakwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ndege kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation kesho dhidi ya Panone Uwanja wa Ushirika.
  Na Jumanne watarudi Dar es Salaam na moja kwa moja kuingia kambini katika hosteli zao za Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA WAENDA PEMBA ‘FASTA’ KUSAKA UBANI WA KUILEWESHA AZAM FC JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top