• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 20, 2016

  MAZEMBA WAICHAPA ETOILE 2-1 NA KUBEBA SUPER CUP

  MABAO mawili ya kipindi cha kwanza ya Daniel Nii Adjei yametosha kuipa TP Mazembe ubingwa wa Super ya Shirikisho la SOka Afrika (CAF) baada ya kuifunga 2-1 Etoile du Sahel ya Tunisia leo Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, DRC.
  Mchezaji huyo wa Ghana alifunga bao la kwanza dakika ya 19 kabla ya kufunga la pili dakika ya 45, wakati Mohamed Msakni aliifungia Watunisi dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza.
  TP Mazembe wakifurahia na taji lao la Super Cup ya CAF Uwanja wa Mazembe leo

  Hilo linakuwa taji la tatu kwa Mazembe la Super Cup, baada ya awali kutwaa Kombe hilo mwaka 2009 na 2010, sambamba na kuendeleza wimbi lake la ushindi tangu ilipotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu aliingia akitokea benchi dakika ya 78 kuchukua nafasi ya Adama Traore kwenye kikosi cha hicho cha mabingwa wa Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAZEMBA WAICHAPA ETOILE 2-1 NA KUBEBA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top