• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 24, 2016

  MESSI HAFAI KABISA! AWAPIGA 2-0 ARSENAL EMIRATES, BAYERN NA JUVENTUS SARE 2-2

  MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi amefunga mabao yote, Barcelona ikiilaza 2-0 Arsenal katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Emirates London.
  Messi amefunga mabao hayo dakika ya 71 akimalizia pasi ya Neymar wakati la pili alifunga kwa penalti dakika ya 83, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Mathieu Flamini.
  Arsenal sasa watalazimika kupanda mlima katika mchezo wa marudiano mwezi ujao Uwanja wa Camp Nou kwa kushinda 3-0 ili kwenda Robo Fainali.

  Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi akikimbia kushangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza. Anayemfuata ni mchezaji mwenzake, Luis Suarez  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin/Flamini dk82, Ramsey, Oxlade-Chamberlain/Walcott dk50, Ozil, Sanchez na Giroud.
  Barcelona: Ter Stegen, Dani Alves, Pique, Mascherano, Jordi Alba, Busquets, Rakitic, Iniesta, Suarez, Messi na Neymar.
  Mchezo mwinigne wa Ligi ya Mabingwa leo, Bayern Munich imelazimisha sare ya 2-2 na wenyeji Juventus Uwanja wa Juve.
  Kiungo wa Juventus, Paul Pogba (kushoto) akimtoka Nahodha wa Bayern Munich, Philipp Lahm PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Bayern ilitangulia kwa mabao ya Thomas Muller dakika ya 43 na Arjen Robben dakika ya 55, kabla ya Paulo Dybala kuifungia Juve dakika ya 63 na Stefano Sturaro kusawazisha dakika ya 76.
  Bayern sasa wanaweza kusonga mbele hata kwa sare ya 0-0 au 1-1 katika mchezo wa marudiano Ujerumani, kwani watanufaika na sharia ya mabao ya ugenini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI HAFAI KABISA! AWAPIGA 2-0 ARSENAL EMIRATES, BAYERN NA JUVENTUS SARE 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top