• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 21, 2016

  ULIMWENGU ALIPOWEKA REKODI YA MTANZANIA WA KWANZA KUINUA SUPER CUP YA CAF

  Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu akifurahia na taji la Super Cup la CAF baada ya kuiongoza timu yake, TP Mazembe kuichapa Etoile du Sahel ta Tunisia mabao 2-1 jana Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Ulimwengu sasa anakuwa mwanasoka wa Tanzania aliyetwaa mataji mengi makubwa ya Afrika, baada ya mwishoni mwa mwaka kuiwezesha Mazembe pia kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika. Na ndiye mchezaji pekee wa Tanzania kutwaa Super Cup ya CAF, huku Mbwana Samatta aliyekuwa naye Mazembe kabla ya kuhamia KRC Genk ya Ubelgiji, akiwa mchezaji mwingine wa Tanzania aliyetwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika. Ulimwengu na Samatta pia ndiyo Watanzania pekee waliocheza Klabu Bingwa ya Dunia 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ULIMWENGU ALIPOWEKA REKODI YA MTANZANIA WA KWANZA KUINUA SUPER CUP YA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top