• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 25, 2016

  CANNAVARO: MIMI KURUDI 'FIRST ELEVEN' YANGA PLUIJM ATAJUA MWENYEWE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kwamba mustakabali wake wa kurejea kwenye kikosi cha kwanza anamuachia kocha wake, Mholanzi Hans van der Pluijm.
  Beki huyo wa kati ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba Pluijm ndiye anajua na nani anafaa kuanza katika kikosi cha kwanza cha kwanza cha timu na wachezaji jukumu lao ni kuhakikisha wanakuwa fiti wakati wote.
  Cannavaro ambaye amekuwa nje tangu Novemba mwaka jana alipoumia akiichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ikifungwa 7-0 na wenyeji Algeria katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia, tayari ameanza mazoezi na amesema yuko fiti kurejea uwanjani.
  Nadir Cannavaro (katikati) amesema anamuachia kocha Pluijm mustakabali wake wa kurudi firts eleven Yanga

  Lakini imezuka hofu juu ya uwezekano wa Nahodha huyo kurudi kikosi cha kwanza, hususan baada ya beki Mtogo aliyekuwa anaziba nafasi yake kucheza vizuri muda wote huo, tena akishirikiana na wachezaji tofauti, kwanza Kevin Yondan na mwishoni mwa wiki akacheza pamoja na Mkongo, Mbuyu Twite Yanga ikiilaza SImba 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu yabVodacom Tanzania Bara.
  “Kocha ndiye anayefahamu atanichezeshaje na nitaingia vipi kwenye kikosi cha kwanza, mimi ninachokifanya ni kufanya mazoezi kwa bidii ili kujiweka fiti na ushindani,”alisema Cannavaro.
  Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema haofii ushindani wa nafasi ya kucheza uliopo katika safu ya ulinzi ya Yanga kwa sasa, kwani anaamini juu ya uwezo na nidhamu yake. “Bidii na nidhamu kwenye mazoezi ndiyo silaha peke itakayonifanya nirejeshwe kikosi cha kwanza,”amesema. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CANNAVARO: MIMI KURUDI 'FIRST ELEVEN' YANGA PLUIJM ATAJUA MWENYEWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top