• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 25, 2016

  BENDI YA THT KUPAMBA ONYESHO LA BLOGU YA WANANCHI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BENDI ya muziki wa kizazi kipya THT kesho itakuwa na onesho maalum la sherehe ya miaka mitatu ya Kampuni yetu ya Blogu ya Wananchi Media, itakayofanyika Kilimanjaro Hoteli, Dar es Salaam.
  Akizungumza na waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo. Mkurugenzi wa kampuni hiyo Wiliam Malecela (Le Mutuz), alisema kuwa wameamua kufanya sherehe ya miaka mitatu ya Blogu yao ambayo imepata mafanikio makubwa ndani ya miaka hiyo.
  Alisema licha ya kesho kufanya sherehe yake kwa burudani, leo itakuwa na semina maalum ya vijana 300, ambao watakuwa pamoja na matajiri 6 vijana na vijana watatu viongozi wa wa Kitaifa.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Blogu ya Wananchi Media, Wiliam Malecela (Le Mutuz) akizungumza na Waandishi wa Habari


  Alisema lengo la semina hiyo ni kubadilishana mawazo ya jinsi Matajiri na Viongozi hao walivyopigana mpaka kufikia walipo kimaisha. 
  "Kwa nini Tunasheherekea miaka mitatu? ni kwamba tunashehekea miaka 3 ya kuzaliwa kwa Blogu ya Wananchi MEdia Company Limited, ni kampuni niliyoianzisha Mwaka 2012 kwa kununua Laptop ya USD $ 500 pale GMO Samora Avenue"
  Na Najivunia hili kwa sababu nilianza na kutembelewa na watu 200 kwa siku (Viewers 200 siku) katika miaka mitatu hii blog yangu inatembelewa na watu 70,000 mpaka 100,000 kwa siku ni kitu cha kushukuru wadau kwa kutambua mchango wangu katika mitandao ya kijamii".
  Kampuni hiyo Ilianza wa dola ya Kimarekani 500, ikiwa na usajili wa makampuni wa Brela, na inatoa ajira kwa Vijana 4 waliomaliza Vyuo Vikuu nchini na Kampuni hii ina Ofisi yake katika jengo la Tancot House hapa mjini Sokoine Drive.
  Pia katika miaka 3 tumeweza kuongezeka kutoka matumizi ya Blogspot ya Google mpaka kuwa na Domain yetu wenyewe ya www.williammalecela.com na kuongeza uwepo wetu kwenye Facebook, Twitter, na Instagram ambapo sasa tuna uwezo wa kurusha habari moja ikafika kote kwa wakati mmoja na kutupa nguvu ya kuwafikia watu 500,000 kwa siku.
  Mipango ya baadaye ni kwamba Kampuni hii imewekeza kwenye /kampuni mpya ya Media ya African Swahili Media Radio & TV ambayo tayari imeshapata leseni ya kufungua Radio na TV ambayo inatazamiwa kuwa hewani by April Mwaka huu, kituo cha Radio kitakuwa Morogoro na TV itakuwa Dar. Pia ni matazamio yetu kufanikiwa kutoa ajira zaidi angalau kwa vijana 10.
  "Tunasherehekea ubunifu ambao ni muhimu kwa sana kwa Vijana wetu wanaomaliza Vyuo Vikuu na Shule zetu kwa ujumla kwamba wanapomaliza Shule wasisubiri kuajiriwa na Serikali kwa sababu ajira hazipo tena, isipokuwa wapigane na kujiajiri wenyewe kwa kutumia ubunifu wa binafsi".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BENDI YA THT KUPAMBA ONYESHO LA BLOGU YA WANANCHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top