• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 27, 2016

  LEICESTER CITY HAIKAMATIKI ENGLAND, CHELSEA NAYO 'YAFUNGULIA MBWA'

  RATIBA NA MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND
  Leo Februari 27, 2016  
  West Bromwich Albion 3-2 Crystal Palace
  Leicester City 1-0 Norwich City
  Stoke City 2-1 Aston Villa
  Watford 0-0 Bournemouth
  Southampton 1 - 2 Chelsea
  West Ham United 1-0 Sunderland
  Kesho; Februari 28, 2016
  Tottenham Hotspur Vs Swansea City (White Hart Lane, Saa 11:05 jioni)
  Manchester United Vs Arsenal (Old Trafford, Saa 11:05 jioni)

  Leonardo Ulloa akishangilia bao lake la dakika ya 89 lililoipa Leicester ushindi wa 1-0 dhidi ya Norwich leo  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  BAO pekee la Leonardo Ulloa dakika ya 89, limeipa Leicester City ushindi wa 1-0 dhidi ya Norwich City Uwanja wa King Power katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.
  Ushindi huo unaifanya Leicester izidi kukwea kileleni mwa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 56 baada ya kucheza mechi 27, ikiwazidi kwa pointi tano wote, Tottenham Hotspur na Arsenal wanafuatia, wakiwa wamecheza mechi 26. 
  Spurs kesho wanaikaribisha Swansea City Uwanja wa White Hart Lane, wakati Arsenal wanaifuata Manchester United Uwanja wa Old Trafford.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Chelsea imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Southampton Uwanja wa St. Mary's, mabao yake yakifungwa na Cesc Fabregas dakika ya 75 na Branislav Ivanovic dakika ya 89, baada ya wenyeji kutangulia kwa bao la Shane Long dakika ya 42.

  Branislav Ivanovic (kushoto) akienda juu zaidi ya Virgil van Dijk kuifungia Chelsea bao la ushindi kwa kichwa dakika ya 89 leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  West Bromwich Albion imeshinda 3-2 dhidi ya Crystal Palace, mabao yake yakifungwa na Craig Gardner dakika ya 12, Craig Dawson dakika ya 20 na Saido Berahino dakika ya 31, huku ya wageni yote yakifungwa na Connor Wickham dakika ya 48 na 80 Uwanja wa The Hawthorns.
  Mabao mawili ya Marko Arnautovic kwa penalti dakika ya 51 na 56, yameipa Stoke City ushindi wa 2-1 dhidi ya Aston Villa, ambayo bao lake limefungwa na Leandro Bacuna dakika ya 79 Uwanja wa Britannia, wakati bao pekee la Michail Antonio dakika ya 30, limeipa 27 West Ham United ushindi wa 1-0 dhidi ya Sunderland Uwanja wa Boleyn Ground na Watford imetoa sare ya 0-0 na Bournemouth Uwanja wa Vicarage Road.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LEICESTER CITY HAIKAMATIKI ENGLAND, CHELSEA NAYO 'YAFUNGULIA MBWA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top