• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 28, 2016

  CABALLERO AOKOA PENALTI TATU ZA LIVERPOOL, MAN CITY YATWAA CAPITAL ONE KWA MATUTA

  MANCHESTER imetwaa Kombe la Ligi England, maarufu kama Capital One Cup baada ya kuifunga kwa penalti 3-1 Liverpool usiku huu Uwanja wa Wembley kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.
  Shujaa wa Man City leo alikuwa ni kipa Willy Caballero aliyeokoa penalti tatu na kukipa taji la Capital One kikosi cha Manuel Pellegrini, baada ya kiungo Yaya Toure kufunga penalti ya mwisho.
  Emre Can pekee alifunga penalti ya Liverpool, wakati za Lucas, Philippe Coutinho na Adam Lallana zilichezwa na Caballero, huku za City zikitiwa nyavuni na Sergio Aguero, Jesus Navas na Toure, baada ya Fernandinho kukosa ya kwanza. 

  Willy Caballero akiwa amebebwa na wachezaji wenzake wa Manchester City baada ya kuokoa penalti tatu na kuipa timu hiyo taji la Capital One Uwanja wa Wembley PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Fernandinho alianza kuifungia Manchester City dakika ya 49, kabla ya Philippe Coutinho kuisawazishia Liverpool dakika ya 83.
  Kikosi cha Man City kilikuwa; Caballero, Sagna/Zabaleta dk90, Kompany, Otamendi, Clichy, Fernandinho, Fernando/Navas dk90, Silva/Bony dk110, Toure, Sterling na Aguero. 
  Liverpool: Mignolet, Clyne, Lucas, Sakho/Toure dk25, Moreno/Lallana dk72, Milner, Henderson, Can, Coutinho/Origi dk80, Firmino na Sturridge. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CABALLERO AOKOA PENALTI TATU ZA LIVERPOOL, MAN CITY YATWAA CAPITAL ONE KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top