• HABARI MPYA

    Thursday, February 18, 2016

    FOWADI SIMBA NA YANGA ZOTE MOTO WA MABAO, JUMAMOSI KAZI IPO TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WAKATI nyasi za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zinatarajiwa kuwaka moto Jumamosi kwa mpambano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga – gumzo kubwa ni safu za ushambuliaji za timu hizo.
    Mashabiki wa Yanga SC wanatembea wakiimba Ngoma na Tambwe – yaani washambuliaji wao wawili wa kigeni, Donald Dombo Ngoma kutoka Zimbabwe na Amissi Joselyn Tambwe wa Burundi.
    Hao ndiyo vinara wa mabao wa timu wakiwa washambuliaji pacha wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu msimu huu. Kwa pamoja, Tambwe na Ngoma wamefunga mabao 24 kati ya 42 yaliyofungwa na klabu hiyo msimu huu.
    Washambuliaji pacha wa Simba SC, Ibrahim Hajib (kulia) na Hamisi Kiiza (kushoto) kwa pamoja wamefunga mabao 24 Ligi Kuu

    Na Tambwe mfungaji bora huyo wa msimu w    a 2013-2014 ndiye anaongoza kwa mabao ndani ya Yanga SC, akiwa amefunga mara 14 akifuatiwa na Ngoma mwenye nabao 10.
    Mashabiki wa Simba SC nao wanatembea wakitambia wakali wao wa mabao Hamisi Friday Kiiza na Ibrahim Salum Hajib ambao kwa hakika msimu huu wanaibeba klabu hiyo.
    Kwa pamoja wawili hao, Mganda Kiiza na mtoto wa nyumbani, Hajib wameifungia Simba SC mabao 24 ya 35 ya timu katika msimu huu wa Ligi Kuu.
    Kiiza ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao kwa ujumla katika Ligi Kuu, akiwa amefunga mara 16, wakati Hajib ana mabao nane.
    Washambuliaji pacha wa Yanga SC, Donald Ngoma (kulia) na Amissi Tambwe kusjoto

    Na hata mabeki wa timu zote mbili wanajua wakali hao wanne ndiyo wa kuchungwa zaidi katika mchezo wa Jumamosi kwa sababu ni wachezaji wenye njaa ya mabao.
    Hajib na Kiiza wote bado hawajui ladha ya nyavu za Yanga SC, wakati Tambwe anajua utamu wa kuwafunga Simba SC. Kiiza akiwa Yanga SC aliwafunga sana Simba. Tambwe akiwa Simba pia aliwafunga Yanga. Ngoma na Hajib ndio ambao hawajawahi  kwenye mechi ya watani wa jadi, ambao Jumamosi watataka kuvunja mwiko huo.
    Inajionyesha wazi kabisa, Simba na Yanga ya Jumamosi itakuwa tofauti na Simba na Yanga kadhaa zilizopita miaka ya karibuni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FOWADI SIMBA NA YANGA ZOTE MOTO WA MABAO, JUMAMOSI KAZI IPO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top