• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 28, 2016

  APR YAIFUATA YANGA NA MKWARA MZITO, YAMPA MTU 4-0 NYAMIRAMBO

  Beki wa APR, Abdul Rwatubyaye akikimbia kushangilia na kiungo Yannick Mukunzi baada ya kuifungia hat trick timu yake katika ushindi wa 4-0 jana Uwanja wa Nyamirambo Regional PICHA NA TIMOTH KISAMBIRA, KIGALI

  BAADA ya kutioa Mbabane Swallows ya Swaziland, APR FC ya Rwanda itamenyana na Young Africans, maarufu kama Yanga ya Tanzania katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa kuchezwa kati ya Machi 11 na 12 Uwanja wa Amahoro mjini Kigali, Rwanda wakati mchezo wa marudiano utachezwa wiki moja baadaye mjini Dar es Salaam.
  Beki wa kati, Abdul Rwatubyaye mwenye umri wa miaka 28, amefunga mabao matatu peke yake (hat trick) jana na kiungo Patrick Sibomana akafunga lingine, mabingwa hao wa Rwanda wakikipiku kipigo cha 1-0 walichopewa katika mchezo wa kwanza Swaziland na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1.
  Yanga imefuzu baada ya kuitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya jana kushinda 2-0 Dar es Salaam, ikitoka kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza Mauritius.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: APR YAIFUATA YANGA NA MKWARA MZITO, YAMPA MTU 4-0 NYAMIRAMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top